29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yazipa tano TACAIDS, UN-WOMEN mapambano dhidi ya UKIMWI

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Serikali imepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake (UN-WOMEN) katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI yanafanikiwa.

Hayo yamebainishwa juzi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Kisayansi la Kitaifa Kuhusu VVU na UKIMWI katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Modern Highland, jijini Mbeya, likiwa na kauli mbiu ya “Zingatia Usawa, Tokomeza Ukimwi, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Amesema kutokanana kazi kubwa inayofanywa na TACAIDS pamoja na UN WOMEN katika kutoa elimu ikiwamo kuwaelimisha wanawake juu ya kujitambua, Ukatili wa kijisia ndiyo sababu kumekuwa na matokeo chanya kwa wanawake kujitokeza kupima ili kutambua hali zao.

“Nikiri na kupongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na TACAIDS chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk. Leonard Maboko, kwani tunaona matokeo chanya, na nhiimani ya Serikali kwamba mtaendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kufikia malengo ambayo kama taifa tumejiwekea.

“Lakini pia kipekee niwapongezea UN WOMEN kwa namna ambavyo wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kutokomeza UKIMWI kwani nguvu yao wanayoitoa katika kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wanawake ndiyo imekuwa kichocheo kikubwa cha kundi hilo muhimu kujitokeza kwenye vituo mbalimbali vya afya kwa ajili bya kutambua hali zao.

“Hivyo kipekee niendelee kuwatia moyo TACAIDS na UN WOMEN Tanzania katika kuendelea juhudi hizo lakini pia na wadau wengine kama UN AIDS katika kuhakikisha kuwa jamii yetu inakuwa salama bila maambukizi ya VVU.

“Tunatambua umuhimu wa kundi hili la wanawake na ndiyo sababu juzi tumezindua Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia pale Mlimani City, Dar es Salaam na Rais wetu Samia Suluhu, tayari aamejipambanua na ameweka bayana msimamo wake dhidi ya ukatili wa kijinsia na kusisitiza umuhimu wa kubadili fikra na kufanya harakati zote kwa ushirika kati ya wanaume na wanawake ili kujenga jamii yenye amani upendo na usawa.

“Lazima jamii yetu ijenge msukumo wa kuhakikisha kuwa kila mtu katika nafasi yake anapaza sauti na kuchukua hatua ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ukatili wa kingono kama vile rushwa ya ngono, ukatili baina ya wenza, ubakaji, mimba na ndoa za utotoni, ” amesema Majaliwa.

Kwa kipindi kirefu sasa UN-WOMEN Tanzania imekuwa ikishirikiana na TACAIDS katika kuhakikisha kuwa inawajengea uwezo wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwamo mtazamo wa kijinsia, Ukatili wa kijinisa, msukumo juu ya kupima na kutambua hali zao za maambukizi ya UKIMWI, hamasa juu ya kuchunguza Saratani ya Mlango wa Kizazi hususan kwa wanawake waishio na VVU nchini na kampenhi nyingine nyingi.

Hatua hizo zote na nyingine ndizo zimekuwa zikichochea wanawake kuongoza kufika kwenye vituo vya afya kutambua hali zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles