24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yazindua muongozo huduma za afya kwa jamii

 MWAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM 

SERIKALI imesema kuwa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga, ikiwemo elimu ya afya na uhamasishaji, lishe, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi na afya ya mama na mtoto. 

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa muongozo wa mpango wa huduma za afya katika jamii na matumizi ya dashibodi ya viashiria vya elimu ya afya kwa umma. 

“Hii itasaidia juhudi za kupunguza mzigo wa gharama za matibabu unaowatesa wananchi na kuongeza matumizi ya serikali katika tiba ya magonjwa yanayoweza kuzuilika au kuepukwa,” alisema Ummy 

Pamoja na hali hiyo alisisitiza kuwa umuhimu wa huduma za kinga ambao umezingatiwa katika Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 na Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Mwaka 2015 – 2020 utakuwa kipaumbele katika maandalizi ya Sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2020. 

Mkakati huo wa kutumia watoa huduma za afya kwa jamii utawezesha kuwepo kwa huduma imara za kinga katika ngazi zote ikiwemo utoaji elimu ya afya na uhamasishaji kama njia muhimu ya kusaidia jamii kujikinga na magonjwa. 

“Hii itawezesha Taifa letu kuwa na wananchi wenye afya njema wanaochangia katika maendeleo yao, familia zao, jamii wanayoishi na nchi yetu kwa ujumla,” alisema 

Waziri Ummy alisema kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote yaani Universal Health Coverage ambavyo itajumuisha utoaji elimu ya afya juu ya mambo yahusuyo lishe, afya ya uzazi, watoto na vijana ikijumuisha magonjwa ya mlipuko kama COVID-19 pamoja na magonjwa yasiyoambukiza. 

“Kwa mfano katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita tumeshuhudia ongezeko la idadi ya watu waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukizakutoka watu milioni 3.4 (3,386,067) mwaka 2016 hadi wagonjwa Milioni 4.2 (4,190,467) mwaka 2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24 ya wagonjwa hao,” alisema 

Hata hivyo sambamba na takwimu za wagonjwa, pia tumeshuhudia ongezeko la vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza hadi kufikia asilimia 33 ya vifo vyote nchini kwa mwaka 2017, ambapo jumla ya vifo 134,600 viliripotiwa na kuhusishwa na magonjwa yasiyoambukiza. 

Huku vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu vikichangia kwa asilimia 13, idadi ambayo ni kubwa kuliko ile itokanayo na magonjwa kama Ukimwi, Kifua Kikuu au Malaria. 

Naye Mkurugenzi wa Miradi ya USAID Tulonge Afya, Waziri Nyoni aliipongeza serikali kwa maamuzi ya kuufanya mfumo huu wa wahudumu wa afya wa jamii kwa kuufanya uwe rasmi tofauti na awali ambapo kila mdau alikuwa akitumia mfumo wake hivyo kuwa na changamoto nyingi. 

Alisema kuwa USAID Tulonge Afya, imekuwa ikitumia mfumo wa wahudumu wa afya ya jamii kufanikisha miradi yake mingi ya afya hapa nchini. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles