29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawekeza zaidi ya bilioni mbili kilimo cha Umwagiliaji Simanjiro

Mohamed Hamad – Simanjiro

Serikali imewekeza zaidi ya billion mbili  kuboresha skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna iliyopo Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa lengo la kuwa na uhakika wa chakuka.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi, jana Juni 17, alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kimebadilisha maisha ya wananchi wanaojishuhulisha na kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa na uhakika wa chakula, na kupata kipato cha kuendesha maisha yao.

“Tuna skimu 15 za umwagiliaji hapa Simanjiro, ambazo kubwa ni Lemkuna, Ngage, Nyumba ya Mungu, Kiruani, na Ruvuremiti, ambapo Serikali imewekeza bil 2.2 katika skimu tatu na wadau wengine wamewekeza mbili huku nyingine zikiendelezwa na wananchi wenyewe” amesema Mkurugenzi Myenzi.

Baadhi ya wakulima wa skimu ya Lemkuna akiwepo Theresia Sandres, alisema amenufaika na shughuli hiyo kwa kujenga nyumba ya kisasa, na sasa anasomesha watoto wake tofauti na awali ambapo aliishi kwa kubahatisha maisha.

“Ndugu zangu hii nyumba inayoonekana hapa ya gharama ni yangu nimeipata kutokana na jitihada zangu katika kilimo cha Umwagiliaji Lemkuna” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles