26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawataka wasimamizi wa hospitali, zahanati kufanya uhakiki wa mizani

Na Safina Sarwatt,Hai

Serikali imewataka wasimamizi wa Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati zote nchini kufanya uhakiki wa mizani kwa lengo la kupata vipimo sahihi vya uzito wa watoto wanaozaliwa , wajawazito na wagonjwa wanaopasuliwa.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Kilimanjaro, Dennis Misango, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambapo WMA mkoani hapa wameadhimisha kwa kufanya ukaguzi wa mizani katika Hospitali ya wilaya ya Hai.

“Serikali imeagiza hospitali,vituo vya afya na Zahanati nchini kuhakikisha mizani wanazotumia zinahakikiwa na zile mbovu zinatengenezwa na wakala wa vipimo (WMA), ambapo Maadhimisho ya siku ya vipimo duniani mwaka huu yamebeba ujumbe wa “Vipimo Sahihi kwa afya” na kwamba WMA wamejipanga kukagua mizani zote katika vituo vya afya, Zahanati na Hospitali zote Mkoa Kilimanjaro,”amesema.

Amesema WMA itahakikisha inafanya ukaguzi wa aina zote za mizani ili waweze kujua zinapima na kutoa majibu sahihi ama la…

Amesema mizani lazima zikaguliwe angalau mara moja kila mwaka na zitoe vipimo sahihi ili kuweza kumwepusha mgonjwa na madhara yanayoweza kusababishwa na matokeo ya vipimo visivyosahihi.

“Mtoto anapozaliwa tu lazima apimwe uzito, mjamzito lazima apimwe uzito na mgonjwa lazima apimwe uzito hivyo ni lazima mizani zikakaguliwa na kutengenezwa ili zitoe vipimo sahihi,”amesema Dennis

Amesema kuwa madhara ya mizani ikiwa mbovu hushindwa kutoa vipimo sahihi hivyo kusababisha daktari kutoa dozi ambayo siyo sahihi kwa mgonjwa na huweza kusabisha madhara kwenye afya ya mgonjwa.

“Maktari hutoa dozi kulingana na uzito wa mgonjwa,hivyo ni lazima vipimo hivyo viwe vinatoa vipimo vilivyosahihi,”amesema.

Aidha, katika hospitali ya wilaya ya Hai wamekagua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) mizani nne ambapo tatu zimebainika kuwa na changamoto,kliniki ya watoto mizani tatu,mbili zinachangamoto, jengo la upasuaji mzani moja haina tatizo na akina mama wanaojifungua na wodi ya wanaume .

Amesema WMA chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekeza itaendelea kutoa elimu kwa watumishi wa sekta ya afya ili waweze kutumia mizani zilizo sahihi.

Amesema lengo ni kuwawezesha watumishi wa afya kutambua mizani iliyosahihi kwa ajili ya vipimo vinavyoruhusiwa kwa afya.

Muuguzi Mfawidhi hospital ya Wilaya ya Hai, Fortunatus Kisheo alisema walikuwa hawatambui baadhi ya mizani wanazotumia ni mbovu na kwamba hazitoi vipimo sahihi.

Amesema WMA mkoani hapa imewaelimisha namna ya kutambua mizani mbovu na kuwaomba kuendelea kutoa ushirikiano wa kufanya ukaguzi wa mizani mara mbili kwa mwaka badala ya kusubiri maadhimisho ya siku ya vipimo duniani.

“Kwa kweli tulikuwa hatutambui mizani mbovu sasa tumegundua baadhi ya mizani ni mbovu zinakata hadi gramu 300 na hi ni hatari kwa usalama wa afya na maisha ya watu,”alisema na kuongeza wilaya ya Hai inavituo, Zahanati na hospiali zote mizani zake zinahitaji kukaguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles