25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawaonya wakurugenzi halmashauri

Allan Vicent -Tabora

SERIKALI imeonya wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuacha mara moja tabia ya kuchepusha fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na wahisani katika maeneo yao.

Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, alipozungumza na wakuu wa wilaya na watendaji wa Serikali mkoani Tabora hivi karibuni.

Alisema fedha zote zinazoletwa na wahisani kusaidia utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya Serikali katika halmashauri husika, zinapaswa kutumika kwa lengo lililokusudiwa.

Alitoa mfano wa fedha zilizotolewa na Serikali ya Uingereza kwa utekelezaji mpango wa uboreshaji elimu katika mikoa tisa kupitia mradi wa Education Quality Improvement Program (Equip Tanzania), imebainika baadhi ya halmashauri zikiwamo za Bahi na Mpwapwa, zimetumia fedha hizo kinyume na lengo.

Alisema wakurugenzi wote waliochepusha matumizi ya fedha hizo, waliitwa na kupewa onyo kali.

Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wakuu wake wa wilaya kwa kusimamia mradi huo vizuri.

“Nawapongeza Tabora kwa kusimamia vizuri mradi wa Equip na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa maofisa wa mradi, madarasa na vyoo vilivyojengwa ni vya kiwango cha juu sana, nimeridhika,” alisema.

Alisema miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za Serikali au wahisani, inapaswa kusimamiwa ipasavyo.

Naye, Mwanri alimhakikishia Jafo kuwa atasimamia maelekezo hayo kwa vitendo, ikiwamo kuhakikisha halmashauri zote zinatenga bajeti ili miradi hiyo iwe endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles