30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawahimiza wawekezaji kilimo cha kahawa kuongeza uzalishaji

Na Upendo Mosha, Dodoma

Serikali imewataka wawekezaji wa Kilimo cha Kahawa nchini kuongeza uzalishaji wa zao hilo hatua ambayo itasaidia kumudu soko la kahawa duniania na kuimarisha bei ya zao hilo ambayo inayumba.

Hayo yalibainishwa na na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba, wakati akifungua kongamano la wadau wa kahawa nchini, lililofanyika Mkoani Dodoma, ambapo lililoandaliwa na Bodi ya kahawa nchini (TCB).

Amesema uzalishaji wa kahawa nchi kwa mwaka ni tani elf 68,000 huku katika nchi ya Uganda uzalishaji ukiwa tani laki 400,000 kwa mwaka jambo na kwamba wawekezaji wanawajibu wa kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wenye tija wa kahawa.

“Mahitaji ya kahawa yetu katika soko la dunia ni makubwa, Uganda wanazalisha zaidi ya tani 400,000 kwa mwaka na sisi tunazalisha zaidi ya tani 68,000 tu licha ya nchi yetu kuwa na maeneo mengi yanayofaa kilimo cha kawaha ni wajibu wenu wawekezaji kishirikiana na serikali katika kuongeza uzalishaji,” amesema Mgumba.

Aidha, amesema kwa sasa serikali imebaini changamoto zinazosababisha tija ndogo katika uzalishaji wa zao la kahawa nchini jambo ambalo limekuwa likisababisha vijana wengi kushindwa kulima kahawa kutokana na kuona kilimo hicho hakilipi.

Mbali na hilo amesema serikali ipo tayari kulinda mikataba ya kilimo kwa wawekezaji na wakulima wa mazao mbalimbali jambo ambalo litabadilisha dhana ya wawekezaji kuitwa madalali wa mazao.

“Kumekuwepo na changamoto kubwa yakuwaona wazalishaji wa kahawa hapa nchini ni kama madalali na walanguzi wa kahawa suala hili limekuwa likiwakatisha tamaa na wakulima kuacha kulima kwa wingi zaidi zao hilo sasa niwahakikishie serikali italinda na kuheshimu mikataba.

“Wenye nia hiyo ya kuwaita wawekezaji madalali wa kahawa muache kwaniwawekezaji ndiyo wenye fursa kubwa ya kuhakikisha zao la kahawa Tanzania linakuwa kubwa zaidi katika uzalishaji wenye ubora katika masoko mbalimbali duniani,”amesema Mgumba.

Mwenyekiti wa bodi ya kahawa Tanzania, Prof. Aurelia Kamuzora amesema wawekezaji ndiyo watakaowezesha kuongezeka kwa tafiti la zao la kahawa hapa nchini pamoja na uwekezaji wa teknolojia ya kisasa itakayoweza kukidhi viwango vya ubora na wingi wa kahawa katika masoko ya ndani na nje ya nchi na kuwaajiri watanzania wengi zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini (TCB), Primus Kimaryo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini (TCB), Primus Kimaryo, amesema bei ya kahawa katika soko la dunia bado inaendelea kuyumba na kwamba pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo serikali hataweza kuweka kinga a bei ya zao hilo kutokana na kwamba kufanya hivyo kutasababisha kahawa ya Tanzania kudoda katika soko la dunia.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Rungwe, Nason Chinai, amesema wakulima wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa pembejeo bora ikiwemo viuatilifu jambo ambalo limekuwa likichangia wakulima kushindwa kulima kwa tija.

“Wakulima tumekuwa tukilima zao hilo kwa gharama kubwa sana jambo hilo linasababisha sisi kushindwa kumudu bei ya kahawa katika soko la dunia na utafiti ndio uhai wa zao hili…tunaomba watafiti muendelee katika utafiti mtuletee mbegu zinazoweza kukindana na magonjwa,”amesema Chinai.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini (TCB), Primus Kimaryo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles