27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa vitambulisho kwa wajasiriamali milioni 1.6

Na Ramadhan Hassna, Dodoma

Serikali imesema hadi sasa imetoa vitambulisho vya wajasiriamali milioni 1.6 kati ya milioni 3.7 vinavyotakiwa kutolewa nakwamba mikakati iliyopo ni jinsi ya kuwafikia milioni 2.1 waliobakia.

Hayo yameelewa jijini Dodoma leo Jumanne Februari 22, 2022 na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula, wakati akifungua kikao viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wake kutoka Mikoa 26 nchini.

Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.

Dk. Chaula amesema Januari 25, mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alipokea changamoto na mafanikio wanayokutana nayo.Amesema kupitia kikao hicho Rais Samia aliagiza kwamba wamachinga ni kundi maalum na sasa liwe chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Amesema taarifa aliyonayo ni kwamba mpaka sasa vimetolewa vitambulisho milioni 1.6 vya wajasiriamali kati ya vitambulisho milioni 3.7 ambapo amedai mikakati iliyopo kwa sasa ni jinsi ya kuwapatia vitambulisho vyao wajasiriamali milioni 2.1 waliobaki.

“Lakini taarifa niliyonayo tunawamachinga milioni  3.7 sasa tunataka hawa waliobaki  milioni 2.1 tunawapaje vitambulisho sasa ndio maana tunatembea na wenzetu wa Tamisemi  watuambie mchakato unaendaje.Kitambulisho ni jambo jema hata sisi ofisini tuna vitambulisho kwahiyo kitambulisho kinakutambua wewe ni nani na upo wapi lile tutaliboresha,”amesema Dk. Chaula.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju.

Kuhusiana na kuwatambua wamachinga Dk. Chaula amesema: “Uzuri mifumo  ya serikali ni endelevu hivyo suala la kutambuliwa sio kwamba walikuwa hawatambuliwi, walitambuliwa na walipata usaidizi wote unaostahili isipokuwa kwa sababu imeanzishwa wizara mpya yenye mambo mahsusi,”.

Kuhusu mgawanyo wa Sh bilioni 5 zilizotolewa na Rais Samia suala hilo Ofisi ya Rais TAMISEMI wanaendelea kulishughulikia.

“Ule mgawanyo uliishatolewa kwa ajili ya kuonesha miundombinu na mchakato unaendelea nina imani tukimaliza haya tutajua tunatokaje Tamisemi wataendelea na uratibu,” amesema Dk. Chaula.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju amesema lengo la kikao hicho cha siku mbili nikupokea kundi hilo kutoka TAMISEMI walikokuwa wakihudumiwa awali kabla ya rais kuagiza liwe chini ya wizara hiyo.

Amesema ndani ya siku mbili watapitishwa katika masuala ya uongozi, taratibu za kiuongozi na namna wanavyoweza kujiongoza kuanzia masoko mpaka taifa, mifumo na mbinu mbalimbali za mawasiliano ikiwemo sheria, taratibu na kanuni za kuongoza umoja wao.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Taifa, Ernest Matondo amesema wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu katika masoko kutokuwa rafiki ambapo ameomba fedha walizopewa zaidi ya Sh bilioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu hiyo ili waweze kufanya biashara katika mazingira mazuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles