Serikali yatoa ukomo kukaimu nafasi kwa watumishi

0
1384

Mwandishi Wetu -Singida

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwajelwa, alisema Serikali baada ya kugundua kuwapo kwa uozo kwa watumishi mbalimbali wanaokaimishwa nafasi waliamua kuja na waraka unaoelekeza kikomo cha mtumishi kukaimu katika nafasi husika.

Dk. Mwanjelwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Suala la kukaimu kwa muda mrefu ndiko kuna sababisha kuwepo na uozo mkubwa katika sehemu zetu za kazi  kutokana na watendaji hao kutokuwajibika kwa ufanisi,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Aliwataka watumishi wote wa halmashauri, hususani mkurugenzi na wakuu wa idara kufanya kazi kwa ushirikiano, ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri wa kitaalamu unaotolewa na alisisitiza suala la mafunzo katika kazi ili kuwaongezea ujuzi watumishi hao.

Katika ziara hiyo mbali na kukutana na kutatua kero mbalimbali za watumishi katika halmashauri za Mkoa wa Singida, pia anapitia kuangalia utekelezaji wa Mpago wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here