31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATOA TAHADHARI YA EBOLA

Na TAUSI SALUM-DODOMA


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekiri kupata taarifa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Akizungumza   mkoani hapa jana, Waziri Ummy alisema  wamepata taarifa hiyo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ugonjwa huo umethibitika kupitia vipimo vya maabara baada ya kutokea wagonjwa 21 na 17 kati yao wamefariki dunia.  .

Alisema ugonjwa huo umetokea katika mjini Biroko,   Jimbo la Equator ambako takribani mwaka mmoja uliopita ulitokea mlipuko mwingine ambao uliua watu wanne.

“Ugonjwa wa Ebola ni hatari na unasambaa kwa kasi na kuleta madhara makubwa kwa afya duniani (Public Health Emergence of International Concern), lakini hadi sasa hapa nchini hakuna mgonjwa aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya ebola,“alisema Ummy.

Alisema Tanzania inapakana na   DRC na ipo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa watu hasa wasafiri wanaotoka na kuingia nchini.

Alisema Wizara inatoa tahadhari ya ugonjwa huo kwa mikoa yote hasa inayopakana na nchi jirani ya Kongo DRC ambayo ni Mwanza, Katavi, Kigoma, Songwe na Rukwa.

Dalili za ugonjwa huo huanza kuonekana kwa mtu aliyeambukizwa baada ya siku mbili hadi 21 na dalili zake ni pamoja na kupata homa kali ghafla, mwili kulegea, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa na vidonda kooni, kutapika, kuharisha   na kutokwa damu nyingi ndani na nje ya mwili.

Ili kujikinga na ugonjwa huo ni kuepuka kugusa mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka kwa mgonjwa wa ebola ikiwa ni pamoja na kuepuka kushughulikia maiti yake na badala yake kutoa taarifa kwa uongozi wa kituo chochote cha huduma za afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles