27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa milioni 10 kusaidia waathirika wa mvua Tanga

Amina Omari, Tanga

Ofisi ya Waziri Mkuu, imetoa msaada wa Sh milioni 10 kwa waathirika wa mvua zilizonyesha hivi karibuni wilayani Korogwe mkoani hapa.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa (OWM) Kanali Jimmy Matamwe amesema msaada kwa ajili ya kusaidia kaya ambazo makazi yao yameharibika kutokana na mvua zilizonyesha na kuleta athari mbalimbali ikiwemo uharibifu wa miundombinu.

Ametaja msaada huo kuwa ni mabati 200, magodoro 100, mikeka 200, ndoo 200 na blanketi 200.

“Pamoja na msaada huu, pia tumekuja kukagua hatua za urejeshaji wa hali baada ya maafa ya mafuriko ya mvua mkoani hapa,” amesema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Shigela amemuomba Kanali Matamwe kuwasaidia kuwajengea uwezo kamati za maafa za mikoa na wilaya ili waweze kukabiliana na majanga kwa weledi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles