29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa maagizo viwanda vya ndani

ELIYA MBONEA-ARUSHA

SERIKALI imewataka wamiliki wa viwanda nchini kutumia fursa ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vinatakavyokithi mahitaji ya soko la ndani.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Nishati Dk. Merdad Kalemani, mbele Kamati ya Bunge ya Bajeti iliyotembelea kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha TANELEC.

Akizungumza mbele ya Kamati hiyo, Waziri Dk. Kalemani alisema, maagizo ya Rais Dk. John Magufuli kuhusu bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani kupewa kipaumbele ni fursa pana kwa wafanyabiashara.

Akitolea mfano huo kwa wafanyabiashara hao alisema baada ya Serikali kupiga marufuku uagizaji wa Transfoma nje badala zinunuliwe kwenye viwanda vya ndani limekuwa na neema kwa kiwanda cha TANELEC.

Alisema mpaka sasa TANELEC ndio wanaowauzia Kandarasi wote wa miradi ya REA na mahitaji mengine, hivyo kutengeneza Transfoma 14,000 kwa mwaka ikilinganishwa na 7,000 zilizotengenezwa miaka iliyopita.

“Tangu msisitizo uwekwe hali imebadilika TANESCO na wakandarasi wengine waliagiza Transfoma India, China na kwingineko, baadaye serikali iliweka msisitizio leo matunda yanaonekana.

“Transfoma moja ilinunuliwa nje kwa Sh milioni 9 na wakati mwingine inakuwa haina kiwango bora, sasa TANELEC wameshusha bei wanauza Sh milini 6 uamuzi wa kuzuia zisiagizwe uliwaumiza, chukiza watu wengi,

“Ukiangalia vizuri utagundua TANELEC ilishakufa kama si ujio wa uchumi wa viwanda hapakuwa na kiwanda hapa,” alisema Dk. Kalemani.

Aidha Waziri Dk. Kalemani aliwaomba kuanza kulipa gawio serikalini kutokana na asilimia 30 za hisa za kiwanda hicho kumilikiwa na Serikali.   

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANELEC Zahir Salehe aliomba Serikali na wabunge wa kamati ya Bajeti kutengeneza mazingira yatakatowezesha bidhaa kama Transfoma kutoka nje zinatozwa ushuru wa asilimia 40 ili kulinda bidhaa za ndani.

Salehe aliendelea kueleza kwamba tayari kampuni hiyo ilishaanza kutoa gawio serikalini ambapo kwa mwaka j

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles