25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa Bilioni 199 kuwezesha mawasiliano vijijini

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imetoa ruzuku ya Sh bilioni 199 kwa ajili ya kuwezesha kampuni za mawasiliano kujenga minara ya mawasiliano 1,087 katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654 vyenye wakazi zaidi ya milioni 15.

Hayo yameelezwa Februari 13,2023 na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli zinazofanywa na mfuko huo.

Mkurugenzi huyo amesema utaekeleza unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 ili kurahisisha matumizi ya mtandao.

Aidha, Mashiba ameeleza kuwa kwa kuhakikisha mfuko huo unafikisha mawasiliano kwa watanzania waishio vijijini wameona vyema kujenga minara hiyo na ikikamilika watanzania waishio vijijini wapatao zaidi ya milioni 15 wataweza kupata mawasiliano ya intaneti kwa uhakika.

“UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654,wakazi 15,130,250 minara 1087 yenye vijiji 3378 na wakazi 13,32,0750 utekelezaji unaendelea katika minara 155 yenye jijiji 276 na wakazi 1,809,500 na tayari ruzuku iliyotolewa ni Sh bilioni 199,

“Pia tayari ruzuku ya Sh bilioni 6.9 imeshatolewa katika mradi wa kimkakati wa Zanzibari ambapo minara 42 katika sheria 38.

Pia amesema kuwa mfuko huo umetekeleza mradi wa kupeleka vifaa vya tehama katika shule 811 na kwa wastani wa shule upewa kompyuta 5, printa 1 na projekta 1.

Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 shule 150 zitafikishiwa vifaa vya Tehama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles