27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATANGAZA MWONGOZO MPYA WA USANIFU BARABARA ZINAZOPITISHA MAGARI MACHACHE

Na Esther Mnyika

Serikali imetangaza mwongozo mpya wa usanifu na ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache hususani vijijini ambao utasaidia kupunguza gharama za ujenzi .

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, alisema mwongozo huo unatoa maelekezo kwa wanaotengeneza barabara za vijijini.

Nyamhanga alisema mwongozo huo utasaidia kupunguza gharama za ujenzi na usalama wa barabara tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanatumia gharama kubwa.

“Kipindi cha nyuma  Wizara ilikuwa inatumia miongozo ya barabara kuu na  za Mikoa  na miongozo  hii ina gharama kubwa kutokana  na kukosa  mwongozo wa barabara zinazopitisha magari  300 kwa siku hivyo  kuepuka gharama hizi tukaanda muongozo huu,”alisema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha aliwataka wahandisi na mafundi ujenzi watumie mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.

ALiongeza kuwa, barabara za vijijini zilikuwa hazina miongozo hivyo walikuwa wanatumia miongozo ya barabara  hizo ambazo kwa siku zinapitisha magari 20,000 hadi 15,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles