28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

SERIKALI YATAIFISHA KIWANDA CHA NYAMA

Na KADAMA MALUNDE- SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga imekitaifisha kiwanda cha nyama kilichopo Old Shinyanga kilichokuwa kinamilikiwa na mwekezaji raia wa kigeni kijulikanacho kama Triple ‘S’.

Inadaiwa kuwa zaidi ya miaka 10 kiwanda hicho hakijawahi kufanya kazi iliyotarajiwa.

Serikali ilimuuzia kiwanda hicho mwekezaji huyo tangu mwaka 2007 ili kukiendeleza kwa biashara ya kuchinja mifugo na kuuza nyama ndani na nje ya nchi, kukuza uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla lakini matarajio hayo hayakufikiwa.

Akizungumza kiwandani hapo jana, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack, alisema kiwanda hicho kwa sasa kitakuwa chini ya Serikali baada ya mwekezaji wake kukiuka masharti na kukitumia kwa mambo yake binafsi.

"Natamka kuanzia sasa kiwanda hiki kipo chini ya serikali na walinzi wote mliopo hapa ondokeni jeshi la polisi ndiyo litakilinda mpaka pale tutakapopata mwekezaji mwingine ambaye atakuwa mwaminifu",alisema Telack.

Telack alisema Tanzania ya viwanda haiwezi kupatikana endapo kutakuwa na wawekezaji wa aina hiyo.

Naye msimamizi wa kiwanda hicho Samweli Kombe alikubaliana na maagizo hayo ya serikali ambapo alidai kuwa atamfikishia taarifa mkurugenzi wake.

Kiwanda cha nyama cha Old Shinyanga mkoani Shinyanga kilijengwa mwaka 1975 kwa lengo la kuinua uchumi wa wafugaji, kupunguza tatizo la ajira, mwaka 2007 serikali ilimpatia mwekezaji ambaye ameshindwa kukiendesha.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles