25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasisitiza umuhimu wa kusajili vyeti vya kuzaliwa, ndoa, talaka

Asha Bani, Morogoro

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Augustine Mahiga amewataka Watanzania kuendelea na kupeleka watoto kujisajili na kupata vyeti vya kuzaliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Dk. Mahiga amesema hayo leo Jumatano Desemba 11, mjini hapa wakati wa uzinduzi wa shughuli ya uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA), ambapo kampeni hiyo pia inaendelea katika Mkoa wa Pwani.

“Mpango wa usajili utaleta mageuzi makubwa kwa kuwa ni haki ya mtoto na kwamba itamsaidia kupata ufunguo wa mambo mengine katika maisha.

“Wazazi wanatakiwa kuwa na kipaumbele cha pekee pale wanapojifungua tu wanatakiwa kuchukua cheti cha kuzaliwa na ni bure kwa kuwa wapo sehemu zote nchini katika maeneo ya huduma ya afya na hata katika ofisi za serikali za kuanzia ngazi za chini mpaka juu,” amesema Dk. Mahiga.

Naye Kaimu Kabidhi Wasihi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson amesema kuna umuhimu wa kusajili watoto na matukio mengine kama vifo, ndoa, talaka ili serikali iwe na takwimu sahihi.

“Tunaposajili vifo pia inakuwa rahisi kwa serikali kufahamu eneo gani lina tatizo na hata kufahamu eneo na idadi ya watu wanaofariki kutokana na maradhi eneo husika,” amesema Emmy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles