27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI KULIWA NA MAMBA

Na Ibrahim Yassin


-Songwe

WANANCHI wa vijiji vilivyopo Kata za Gua na Kapalala wilayani Songwe, wamepongeza hatau ya Serikali kusikia kilio chao cha muda mrefu cha ukosefu wa daraja linalounganisha vijiji vya kata hizo ambao wengi wao waliliwa na mamba.

Akizungumza  jana mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa, mkazi wa Gua, Gasper January, alisema serikali imesikia kilio chao kwa sababu  walikuwa hawana mawasiliano na wakazi wa vijiji vya upande wa pili hasa nyakati za mvua za masika.

January alisema ujenzi wa daraja hilo la kisasa utafungua milango na fursa za kiuchumi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songwe, Abraham Sambira alisema katika Tarafa ya Kwimba, serikali inajenga madaraja makubwa mawili yatakayounganisha vijiji hivyo   na Mkoa wa Katavi.

Alisema daraja la Mto Kikamba linajengwa kwa gharama ya Sh bilioni 1.4 na  Kampuni ya Marts Engineering, litakalounganisha Kata za Gua na Kapalala kwenda mkoani Katavi.

Naye Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo (CCM), alisema ujenzi wa madaraja hayo utakapokamilika utaleta tija za uchumi kwa mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.

Alisema   wananchi wa tarafa hiyo ni wakulima wa mazao mbalimbali hivyo makampuni ya ununuzi yataongezeka.

Naibu Waziri Jenzi., Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, alisema serikali inaendelea kutekeleza na kutatua kero za wananchi.

Alisema  katika nchi nzima yanajengwa madaraja 19 ambayo ana uhakika yatakamilika kwa wakati ikizingatiwa fedha za ujenzi huo zipo.

Hata hivyo alisema ipo haja ya wakandarasi kufanya kazi kwa weledi na kutimiza ujenzi kwa wakati.

Alimtaka mkandarasi anayejenga daraja katika Mto Kikamba  kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles