26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

SERIKALI YASHUSHA MAPATO YA HALMASHAURI

Hadija Omary, Lindi

Mapato ya Halmashauri ya Manispaa Lindi, mkoani hapa yameshuka kutoka Sh bilioni 1.9 mwaka 2015/16 hadi bilioni 1.7 mwaka 2017/18 kutokana na vyanzo vikuu vya mapato kuchukuliwa na serikali kuu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemange wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilayani humo.

Ndemanga amesema kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2015/16  na mwaka 2017/2018 mapato ya ndani ya halmashauri yameshuka kutokana na vyanzo vikuu kutwaliwa na serikali kuu ili kuongeza ufanisi zaidi wa ukusanyaji.

“Mwaka 2015/16 makisio ya mapato yalikuwa 2.4 makusanyo halisi yalikuwa ni 1.9 sawa na asilimia 80 wakati mwaka 2016/17 makisio yalikuwa 1.3 mapato 1.2 na 2017/18 makisio 1.8 na mapato 1.7.

“Niwatoe hofu wajumbe wa mkutano huu kuwa halmashauri  inaendelea na itaendelea kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani sambamba na uanzishwaji wa vyanzo vipya vya mapato ili kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles