28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaridhishwa na nyumba za WHC

Na Faraja Masinde Dar es Salaam

Serikali imeridhishwa na nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Nyumba ya Watumishi Housing Company (WHC), zilizoko katika miradi yake ya Magomeni (Usalama), Kigamboni Gezaulole na Bunju jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa juzi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi Dk. Laurean Ndumbaro alipotembelea Miradi ya nyumba ya Magomeni na Kigamboni Geza Uloloe jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa (WHC), Dk. Fred Msemwa (Katikati) akimweleza jambo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi Dk. Laurean Ndumbaro alipotembelea Miradi ya nyumba ya Magomeni na Kigamboni jijini Dar es Salaam (Picha na Faraja Masinde).

Alisema kazi kubwa na nzuri imefanyika chini ya WHC kwani nyumba ni nzuri na zinavutia kwa Mtanzania yoyote kukaa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Nimetembelea miradi hii ya Watumishi Housing Company ziara ambayo nilianzia kwenye miradi ya Dodoma na sasa Dar es Salaam, niseme tu kwamba kazi nzuri imefanyika kwani majengo yote yanawapangaji wengine wanunuzi ambao ni watumishi wa Serikali.

“Kwani sote tunajua kuwa kama yasingekuwa majengo haya basi Watumishi na watanzania kwa ujumla ambao wamenunua na kupanga nyumba hizi za WHC wangepata changamoto ya makazi.

“Hivyo niwapongeze sana kwani sisi kama serikali kwa kiasi kikubwa tumaridhishwa na namna miradi hii ilivyotekelezwa,” amesema Dk. Ndumbaro.

Upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa (WHC), Dk. Fred Msemwa mbali na kupokea pongezi hizo alitumia pia fursa hiyo kuiomba serikali kuipatia eneo la Magomeni Kota lenye takribani ekari 4 kwa ajili ya kujenga nyumba za Watumishi na Biashara.

Dk. Msemwa amesema iwapo serikali itawapatia eneo hilo wataweza kujenga Magorofa nane (8) ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya familia 700 na hivyo kisaidia Watanzania wengi kupata makazi bora kwa gharama nafuu.

“Kwa nza kabisa tunashukuru sana kwa kuvutiwa na kuridhishwa na miradi yetu hii, lakini pia Katibu Mkuu maombi yetu kwa Serikali ni kupatiwa sehemu ya eneo la Magomeni Kota ambalo limebaki baada ya mradi wa TBA (Walaka wa Majengo wa Serikali) kukamilika, hivyo iwapo tutapata eneo hilo lenye kubwa wa ekari Nne tutaweza kujenga Magorofa nane ambayo yatakuwa na uwezo walichukia familia 700 kwa wakati mmoja.

“Hii ni wazi kuwa itasadia Watanzania wengi wakowemo Watumishi wa Umma kupata makazi bora kwa gharama nafuu zaidi.

“Lakini pia ikizingatiwa kuwa WHC hatuna mkopo wowote ambao tunadaiwa kupitia Miradi yetu yote, hivyo fedha za kuanzia zipo,” amesema Dk. Msemwa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi Dk. Laurean Ndumbaro, akiangalia eneo la Magomeni Kota ambalo WHC imeomba kujenga nyumba zitakazochukua familia 700 (Picha na Faraja Masinde)

Kuhusu maombi hayo, Katibu Mkuu, Dk. Ndumbaro alisema kuwa serikali itaangalia maombi hayo na kwamba iwapo WHC itakidhi vigezo basi itapatiwa eneo hilo.

“Sawa nimepokea maombi yenu, tutakaa tuangalie tuone kama mtakuwa mmekamilisha kila kitu basi hakutakuwa na shida,” amesema Dk. Ndumbaro.

Upande wa Wapangaji wa nyumba hizo akiwemo, Dk. Mayaka Peter wameishukuru WHC na serikali kwa ujumla kwa namna walivyonufaika na miradi hiyo.

“Tunashukuru kwamba nyumba hizi zimetuondolea adha kubwa ya kamakazi kwani hata watumishi wa umma kwa sasa wanatekeleza majukumuyao bila wasiwasi, hivyo ni jambo la kupongewa kwa WHC na serikali kwa ujumla.

“Kwani pia hata changamoto za wakazi wa hapa zimekuwa zikitatuliwa kwa wakati na kupewa kipaumbele,” alisema Dk. Mayaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles