28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaridhishwa na mfumo wa uagizaji mbolea

Mwandishi wetu

Serikali imeelezea kuridhishwa na mfumo wa uagizaji wa mbole kwa pamoja licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zikiwemo za ucheleweshaji wa mbolea kuwafikia wakulima ikiwa ni pamoja na suala la bei elekezi.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa mjini Morogoro na Afisa Kilimo Idara ya Mazao Kitengo cha Pembejeo kutoka Wizara ya Kilimo, Joseph Lyafwila wakati wa warsha ya wadau wa sekta ya kilimo iliyokuwa ikiangazia matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu mfumo wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.

“Kwetu kwenye sekta ya kilimo mfumo huu ni mpya na tayari  tumeona mafanikio yake ndani ya kipindi cha miaka mitatu, hivi sasa mbolea inafika nchini kwa wakati na wakulima pia inawafikia kwa wakati na kama nilivyosema ni ukweli kwamba bado kuna changamoto kadhaa,”.

“Tunajua pia wakulima wamekuwa wakilalamikia suala la bei na hii inatokana na ukweli kwamba kuna baadhi ya vijiji viko mbali sana na inafanya bei inapanda kidogo inagwa serikali bado inangalia changamoto zote  zinazoendelea kujitokeza katika mfumo huu ili tuweze kuzishughulikia “ amesema Lyafwila.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka Baraza la Kilimo, Timothy Mmbaga amesema kuwa waliamua kufanya utafiti huo kuhusu maendeleo ya mfumo ili kuona namna inavyoweza kuishauri Serikali namna bora zaidi ya kuendelea na mfumo huo.

“Kabla ya mfumo huu kulikuwa na changamoto nyingi sana watu walikuwa wanauziwa mbolea feki wengine walikuwa wanauziwa hadi siment, lakini Baraza la Kilimo tulipiga sana kelele na tunaishukuru Serikali ililiona hili na hatimaye kuja na mfumo huu,

“Tunajua mahitaji ya mbolea kwa sasa yanazidi kuongeka hivi sasa inakadiriwa kufikia tani laki nne ingawa kupitia mfumo huu ni tani 70,000 pekee ndio inayoagizwa ingawa tunajua kuna njia nyingine nyingi za uagizaji wa mbolea zaidi ya DAP na UREA zinazoagizwa kupitia mfumo huu” amesema Mmbaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles