32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapongezwa kwa kusikiliza hoja za CWT

Gratian Mukoba
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania, Gratian Mukoba

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimeipongeza Serikali kwa kukubaliana na hoja yao ya kuwa na mwajiri mmoja.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema wamefurahishwa na Serikali kukubali kuunda chombo kimoja cha kuwaajiri walimu nchini.

Alisema CWT ilidai uwepo wa mwajiri mmoja kwa walimu tangu Serikali ya Awamu ya Tatu ili iwe rahisi kutatua kero za walimu nchini.

“Rais Benjamin Mkapa, alisema angemwachia rais wa awamu ya nne akisema kuwa jambo hili linahitaji mabadiliko ya sera na sheria, Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani tunaamini alikabidhiwa jambo hili ambalo tumekuwa tukilipigania kwa miaka kumi,” alisema Mukoba.

Alisema walimu nchini ni asilimia 64 ya watumishi wote wa umma hivyo walihitaji chombo chao kimoja kitakachosimamia ajira yao kama njia ya kumaliza migogoro ya mara kwa mara.

Alisema kwa kuwa azimio la Bunge limepitishwa, CWT inaishauri Serikali isijifungie ndani peke yake na kutoa chombo hicho bila kuwashirikisha walimu.

“Tunachelea kisijekuwa chombo chenye majukumu yasiyokidhi na kusanifu shida za ajira ya walimu ikiwamo usafiri, mishahara na kiinua mgongo,” alisema Mukoba.

Alisema hatua ya kutawanya majukumu ya walimu katika mamlaka mbalimbali, imesababisha kwa kipindi kirefu walimu kuishi na kero zisizopatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Alisema CWT inashauri chombo hicho kiwekwe katika Katiba Mpya kama ilivyo kwa Kenya ambako chombo hicho kinafanya kazi vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles