33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga ‘stop’ watumishi kuhama Dodoma

Na MWANDISHI WETU-DODOMA

SERIKALI imepiga marufuku watumishi wa umma waliohamia Makao Makuu ya nchi Dodoma kwa gharama za Serikali kuomba uhamisho wa kurejea   Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro.

Alikuwa akifanya mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na   uhamisho wa watumishi wa umma kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Dk. Ndumbaro alisema ofisi yake imekuwa ikipokea barua mbili au tatu kwa siku za watumishi waliohamia Dodoma kuomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na za afya wakati Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ina vifaa vya kisasa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa watumishi hao.

Alisema kabla ya watumishi kuhamia Dodoma, Serikali ilitoa maelekezo kwa waajiri kuwasilisha orodha ya watumishi wenye matatizo ya msingi ili wabaki kwenye vituo vya kazi vilivyopo Dar es Salaam wakiendelea kutekeleza majukumu yao.

“Baadhi ya watumishi waliohamia Dodoma, wamegeuza uhamisho huo kuwa mradi  wa kuwaingizia kipato kwa sababu  baada ya kuripoti Dodoma, ndani ya kipindi kifupi wanaomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam,” alisema Dk. Ndumbaro

Alisisitiza kuwa  kutokana na suala hilo, Serikali imetoa Waraka wa Barua wenye Kumb. Na. CAC 228/257/01/A/53 wa tarehe 25 Septemba, 2018 kuhusu Uhamisho wa Watumishi Waliohamia Dodoma Kutekeleza Uamuzi wa Serikali Kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Waraka huo  unazuia mtumishi aliyehamishiwa Dodoma kwa gharama za Serikali kuomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam mpaka atimize miaka mitatu katika kituo cha Dodoma.

Watumishi wa umma kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli, alilolitoa Julai 25, 2016 wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles