24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga marufuku mikusanyiko

Na Brighiter Masaki

Serikali imepiga marufuku mikusanyiko nchi nzima, huku ikiagiza kuwepo kwa tahadhari  ya corona kwa mkusanyiko  ambao utakuwa wa lazima.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema hatua hiyo inalenga kukabiliana wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, ambalo madhara yake yanaendelea kujitokeza.

Katika taarifa hiyo, Waziri Gwajima amewataka viongozi wa Serikali na wale wa sekta binafsi kuonesha mfano wa namna wanavyochukua hatua kukabiliana na ugonjwa  huo.

Kwa mujibu wa Dkt. Gwajima, idadi ya wagonjwa wa corona imezidi kuongezeka nchini na hadi kufikia tarehe 21 mwezi huu, kulikuwa na wagonjwa 682 wanaopatiwa matibabu kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma.

Pia amewataka wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya chanjo dhidi ya corona, ambayo itatoewa bure na kwa hiari.

Amesema jana Julai 22, wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo, tayari kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya chanjo dhidi ya corona na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles