25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, February 13, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali yapewa kongole kwa kuimarisha ustawi wa wananchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuimarisha ustawi na maendeleo ya Watanzania katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, (katikati) akifuatilia mjadala mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utendaji wa Wizara yake katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara yake, Mary Maganga na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Zuhura Yunus.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatma Hassan Toufiq, wakati akihitimisha kikao cha Kamati hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bungeni jijini Dodoma (Januari 21, 2024).

Kikao hicho kilikuwa ni maalum kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) na Taasisi chini yake kuwasilisha taarifa ya utendaji wake kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba, 2024.

“NSSF, OSHA, WCF na CMA kwakweli kazi mnazofanya zinaonekana pamoja na changamoto chache zilizopo lakini sisi kama Kamati tunaridhika na jinsi mnavyotekeleza majukumu yenu.

“Kwa namna ya pekee nimpongeze Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake makini kwani tunatambua dhima kuu ya Mheshimiwa Rais ni kuhakikisha kunakuwa na ustawi na maendeleo ya Watanzania hususan wafanyakazi katika sekta rasmi na isiyo rasmi.”

Mwenyekiti wa Kamati amefafanua kuwa nia njema ya Rais Samia kuboresha ustawi wa wananchi wake inajidhirisha katika jitihada ambazo serikali yake imekuwa ikizichukua katika kuimarisha mifumo mbalimbali ya usimamizi wa masuala ya msingi yakiwemo masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda (mwenye koti la bluu bahari) akiwa na watendaji wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakifuatilia taarifa ya nusu mwaka ya utendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) iliyowasilishwa katika kikao cha Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Januari 21, 2025.

Aidha, ameupongeza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa kufikia idadi kubwa ya maeneo ya kazi nchini na kuhakikisha kwamba wadau wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu usalama na afya kazini.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Waziri mwenye dhamana ya Masuala ya Kazi, Ridhiwani Kikwete, ameishukuru Kamati hiyo ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri ya kuishauri serikali ili kuhakikisha mipango yake ya maendeleo inafanikiwa.

Akitolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema kupitia uwezeshaji wa serikali, Taasisi yake imejipanga kuendelea kujiimarisha zaidi kiutendaji ikiwemo kuongeza vitendea kazi na kujenga miundombinu bora ya kutolea huduma pamoja na kuongeza uelewa wa wadau kuhusu masuala ya usalama na afya kazini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa mwaka wa fedha 2024/2025 wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa kipindi cha nusu ya mwaka (Julai hadi Desemba, 2024) katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kilicho fanyika Bungeni Jijini Dodoma Januari 21, 2025.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles