SERIKALI imesema itamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote aliyesambaza taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi, ilisema kumekuwapo na taarifa za uongo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha habari kinachosema “kanuni na sheria za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zitabadilishwa’.
Taarifa hizo, zimeanza zimeanza kusambazwa juzi zikidai kuanzia janana kuendelea kutakuwa kuna kanuni mpya za mawasiliano.
“Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hii, ni ya uongo na uzushi,haina ukweli wowote na inalenga kuvuruga wananchi…tunaomba waipuuze.
“Wizara inatoa onyo kali kwa mtu yeyote aliyeanzisha na wale wanaoendelea kusambaza taarifa hii,hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaozusha mambo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Serikali inao mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa kwa kutumia mfumo wa “kielectroniki na hardcopy,’’ ilisema taarifa hiyo.
Lisemwalo lipo nyie mnasalitiana wenyewe siri zinavuja halafu mawaonea watu wasio na hatia mjitathimini