30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAOMBWA KUWAPA WAZEE MIKOPO, PENSHENI 

Na Ashura Kazinja


 

wazee

SERIKALI imeombwa kuingilia kati na kusimamia suala la uchumi kwa wazee wapate mikopo na   pensheni ya kila mwezi  waweze kujikimu katika maisha.

Rai hiyo imetolewa na Ofisa Uhusiano wa Shirika la Kuhudumia Wazee mkoani Morogoro (MOREPEO), Wilson Karuwesa.

Alikuwa akizungumza  kwenye  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari zinazowahusu wazee.

Mafunzo hayo  yaliandaliwa na Helpage International kwa udhamini wa Mfuko wa Conrad Hilton.

Karuwesa alisema  wazee wamekuwa wakipuuzwa katika suala la uchumi kwa vile hata benki zinawanyima mikopo.

Alisema kama sera ni kuhakikisha hakuna anayeachwa katika safari ya utekelezaji wa maendeleo endelevu ipo haja kwa serikali kuhakikisha   wazee hawanyanyaswi,  wanasaidiwa na kuwezeshwa kwa uchumi kwa kupewa mikopo.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Samson Msemembo, alisema maofisa mipango wengi wanakwepa kuweka kipaumbele suala la wazee wakidai  a fedha wanazoletewa ukomo wake hauruhusu kuwaingiza wazee.

Alisema wengine    wanadanganya kwamba serikali kuu ndiyo imeondoa msaada kwa wazee.

Msemembo alisema wazee wanataabika  katika suala la uchumi.

Alisema ipo haja sheria ya wazee ikatungwa  kuwasaidia kuondokana na adha ya kukataliwa wakati wa kutafuta mikopo ya kuwainua kwa uchumi.

Alisema asilimia 50 ya mayatima wanakaa na wazee vijijini na kitendo cha kuwanyima ushiriki wa uwezeshaji ni kuwatesa wao  na watoto wanaowategemea.

“Utakuta mzee kijijini ameachwa na mzigo wa kulea mayatima na anategemewa kwa kila kitu nyumbani, hivyo ukimuwezesha kwa kumuinua kwa uchumi na kumpa pensheni ya kila mwezi utamsaidia kuyamudu maisha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles