26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kutupia jicho sheria ya madeni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI imeombwa kuangalia upya sheria ya madeni ikiwa ni pamoja na kuunda mfumo mpya utakaoshirikisha Bunge katika mchakato wa ukopaji na urejeshaji wa madeni mbalimbali ili kuleta nidhamu na uwajibikaji katika matumizi ya fedha hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TCDD, Hebron Mwakagenda akifafanua jambo kuhusu deni la taifa na athari zake.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali inayofuatilia Madeni na Maendeleo Tanzania TCDD, Hebron Mwakagenda wakati akifungua mkutano huo uliolenga kutoa elimu kwa viongozi hao kuhusu deni la taifa.

Alisema ni vema kukawekwa mifumo mizuri katika ukopaji na urejeshaji wa madeni ili kulipunguzia taifa mzigo wa madeni ambao unaweza kuleta athari ya nchi kudidimia kiuchumi pamoja na kushindwa kutoa huduma muhimu kwa jamii.

“Ifike wakati kukawekwa mifumo mizuri ya ukopaji kwa kulishirrikisha Bunge hii itapunguza ukopaji usio na tija ambao hata ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ‘CAG’ amekuwa akibaini kasoro kadhaa katika ukopaji na matumizi ya fedha hizo za Serikali,” alisema Mwakagenda.

Aliongeza kuwa ni muhimu kukopa kwa tija na fedha hizo zitumike kwa faida ya jamii ya sasa na kizazi kijacho.

Alisema kwa sasa mfumo wa ukopaji umebadilika badala ya kukopeshana nchi kwa nchi imehamia kwenye biashara hivyo endapo kusipowekwa umakoni taifa litadidimia.kiuchumi kwa sababu ya kuelemewa na madeni.

Alisema asilimia 60 ya fedha za serikali zipo kwenye manunuzi hivyo ni muhimu zisimamiwe vema ili zilete matinda katika utoaji huduma.

Alisema TCDD kwa kushirikiana na nchi nne za Afrika Mashariki wamefanya utafiti kuhusu madeni kwenye nchi husika lengo ikiwa ni kujenga uelewa na umuhimu wa uwazi katika nchi hizo.

Naye, Mchungaji wa Kanisa la Kisabato Tanzania, Elisante Jackson alisema Serikali iwe wazi wakati inaingiia mikataba mbalimbali ili kuondoa sintofahamu kwa jamii kuhusu madeni.

Alisema katika kuhakikisha serikali inajenga mahusiano na wananchi wake ihakikishe inaondoa sheria kandamizi ikiwemo ile ya mazingira inayohusu utupaji taka kwakuwa imekuwa ikiumiza wananchi.

Aliomba Serikali izingatie sheria ya manunuzi kwakuwa itasaidia kuondoa kasoro zinazojitokeze kwenye baadhi ya maeneo ya kiutendaji hivi sasa.

Jackson alisema ili kupata kodi za kutosha ni vema serikali ikajenga mahusiano na wafanyabishara kwakuwa itasaidia kuzuia mianya ya ukwepaji kodi.,

“Upo umuhimu wa viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya kitaifa ambao wakishirikishwa ipasavyo katika michakato itasaidia kuinua uchumi wa nchi,”alisema Jackson.

Aliwataka viongozi wa kisiasa kukubali kukosolewa kwani matamko yao wanayoyatoa mara nyingi hayana afya kwa jamij.

Wakati huohuo, Mjumbe wa Bodi ya TCDD, Camilius Kassala kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), alisema viongozi wa dini wana fursa ya kupaza sauti kwa.jamii hasa za madeni na maendeleo ili kutoa maarifa, elimu na hekima.

“Viongozi wa dini kwa pamoja wakishiriki kupaza sauti na kutoa elimu kuhusu ukopaji wenye tija itasaidia kujenga nidhamu kwenye natumizi ya fedha,’ alisema Kassala.

Alisema rushwa na vyanzo vya mapato vikidhibitiwa itasaidia kuongeza uwezo wa kulipa deni la taifa. Kassala alisema upo umuhimu wa kukopa kwa tija na kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles