25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuitangaza Holili kuwa mji mdogo wa biashara

Safina Sarwatt,Rombo

Serikali imeombwa kutangaza rasmi usajili wa kijiji cha Holili kuwa Mamlaka ya mji mdogo wa biashara kutokana na kukidhi sifa na vigezo.

Diwani wa kata ya Holili wilaya ya Rombo, Kelvin Kahangala, ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 14, 2021 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea kata hiyo kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo ya wananchi wa kata hiyo.

Amesema serikali hainabudi kutangaza usaili wa Holili kuwa mamlaka ya mji mdogo wa biashara kutokana na mji huo kufanya biashara kimataifa kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.

Amesema mpango huo ulianza miaka mingi iliyopita na Oktoba 23, 1992 ilitangazwa kwenye gazeti la serikali namba 291 kuwa Holili ni Mamlaka ya mji mdogo wa biashara.

Kahangala amesema Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa akihutubia mkutano wa kampeni wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Septeba 7, 2020 Holili alisema wananchi Holili wanakila sababu za kudai Holili kuwa mamlaka ya mji mdogo wa biashara.

“Mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na kumchagua mgombea wa CCM Kelvini wanaomba SERIKALI kutimiza ahadi lHolili itakuwa mamlaka ya mji mdogo wa kibiashara,” amesema Kahangala.

Amesema Holili ina wakazi zaidi 8,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 na mji unakuwa kwa kasi kubwa huku zikiwemo taasisi mbili mbali za serikali na watu binafsi.

Amezitaja baadhi ya taasisi hizo ni pamoja na kuwa na shule tatu za msingi na tatu za sekondari kuwa na kituo cha polisi.

Aidha, ametaja taasisi nyingine zilizopo Holili kuwa ni huduma za kifedha zikihusisha benki, ofisi za ushuru wa forodha, TBS, Mionzi, Kilimo, Mifugo, Wakala wa Vipimo na huduma nyingine.

Amesema pamoja na Holili kuwa kijiji ardhi yao imepangwa katika mipango miji na ardhi yao imepimwa na wananchi wanalipia Kodi za serikali .

Amesema serikali ina kila sababu za kutangaza Holili kuwa Mamlaka ya mji mdogo wa biashara hatua inayopaswa kwenda sambamba na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa Mamlaka.

Amesema serikali inapaswa kuanza kuweka jitihada katika kuboresha mifumo yote ya uendeshaji wa mamalaka ili kukuza biashara na mji huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles