24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuanzisha vituo vya malezi na makuzi ya watoto

Na Samwel Mwanga, Maswa

SERIKALI kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kuanzisha kuanzisha Vituo vya Malezi na Makuzi ya awali kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi, minne nchi nzima ikiwa ni moja ya mikakati ya kumjenga na kumlinda mtoto.

Hayo yameelezwa mjini Maswa mkoani Simiyu na baadhi ya Wazazi na Walezi wa wanafunzi katika Vituo vya Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto vya Kasajo Day Care na St. Josephine Bhakita wakati wakizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea vituo hivyo kwa nyakati tofauti.

Wamesema kuwa vituo vya malezi na makuzi kwa watoto ni muhimu sana ili kuhakikisha watoto wanapata huduma bora zitakazowezesha uchechemuzi wa bongo zao na kuwekwa katika mazingira mazuri ya ukuaji.

“Hivi ni vituo muhimu unaweza ukadhani ni jambo dogo, hili ni jambo kubwa sana na la msingi katika malezi na makuzi ya awali kwa watoto wetu,” amesema Janeth John.

Waliendelea kueleza  kuwa vituo hivyo ni suluhisho tosha kwa tatizo la malezi na makuzi ya mtoto hasa kwa changamoto za utafutaji kipato kwa wazazi kukosa muda mwingi wa asubuhi mpaka jioni kukaa na watoto wao.

“Vituo vya malezi na makuzi ya awali kwa watoto vinalenga kutoa fursa kwa wazazi na walezi kutekeleza shughuli za kiuchumi,” amesema George Nyagawa.

Naye Mkuu wa  Kituo cha Malezi na Makuzi cha Lusajo,Edward Khija  alisema kuwa  kuwa Kituo hicho kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2018 mpaka mwaka 2020 kimefanikiwa kuwaandaa watoto zaidi ya 200  kabla ya kuwapeleka katika Shule za awali.

“Walimu katika shule tulizowapeleka watoto hao wanasema watoto wanaopatia katika Kituo hiki wanakuwa na uelewa wa haraka ukilinganishwa na watoto amabao hawajapitia katika vituo vya malezi” alisema.

Ameongeza kuwa ujifunzaji kwa watoto umezingatia falsafa za malezi na makuzi ya mtoto zinazohimiza umuhimu wa miaka ya mwanzo ya mtoto kupata uangalizi na malezi bora kwani ni msingi wa maisha ya baadaye.

Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge alisema kuwa kwa umuhimu wa Vituo vya Malezi na Makuzi ya Mtoto ni vizuri taasisi binafsi na za madehebu ya dini kuanzisha vituo hivyo ambavyo kwa sasa vina umuhinu mkubwa katika jamii.

“Kwa mfumo wa serikali elimu inaanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu hivyo ni vizuri kwa jamii hasa sekta binafsi yakiwemo madhehebu ya dini yakaanzisha vituo hivyo vya malezi ya Awali ya Makuzi ya watoto wadogo na serikali ni lazima itoe miongozo juu ya utoaji wa elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa kumuuandaa mtoto kuingia shule ya awali na msingi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles