25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaokoa zaidi ya Bilioni 9 upandikizaji figo Muhimbili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

SERIKALI imeokoa zaidi ya Sh bilioni 9 kwa kupandikiza figo wagonjwa 75 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Agosti 10,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali na mwelekeo wa Hospitali hiyo kwa mwaka 2023-2024 kwa Waandishi wa Habari.

Prof. Janabi amesema katika kipindi cha mwaka uliopita, Hospitali hiyo ilifanikiwa kufanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 7 ambao ulifanyika kwa mara ya kwanza Hospitali ya Mloganzila na kuifanya Mloganzila kuwa Hospitali ya tatu nchini kutoa huduma hiyo tangu ilipoanzishwa Novemba 2017.

Amesema hadi sasa wagonjwa waliopandikizwa wamefikia 75 ambao hugharimu Sh bilionio 2.250 na kama wangeenda nje Serikali ingelipia zaidi ya Sh bilioni 9.

Prof. Janabi amesema katika kutekeleza azma ya kutoa huduma bobezi, kwa nyakati tofauti Hospitali iliendelea kutoa huduma za kibobezi.

Amesema Hospitali iliendelea kutoa huduma ya upandikizaji vifaa vya kusaidia kusikia ambapo wagonjwa 11 walipata huduma hiyo.

“Hadi sasa wagonjwa 59 wamepata huduma hii tangu ilipoanzishwa nchini Juni 2017,”amesema Prof. Janabi.

Amesema Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo kupitia hospitali ya umma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema kama wagonjwa hawa wangeenda nje ya nchi Serikali ingelipa zaidi ya Sh bilioni 5.

Amesema katika kipindi kilichopita, Hospitali ilifanikiwa kuboresha miundombinu yake ili kuweka unadhifu wa maeneo ya kutolea huduma.

Amesema Ukarabati huo ulihusisha Jengo la Wazazi ambapo tayari wodi 33 na 34 zimekarabatiwa kwa udhamini wa benki ya NMB.

Katika jitihada za kupunguza vifo vya kina mama na watoto, Hospitali ilifanikiwa kujenga chumba cha dharura kwa Kinamama Wajawazito ambacho sasa kinasaidia kina mama wanaokuja na rufaa wenye ujauzito kuhudumiwa hapo au kina mama ambao wamejifungua watoto kabla ya umri kufikia hapo.

Amesema katika jengo la Sewahaji, ukarabati mkubwa umefanyika kwa Wodi 17 na 18 na kuwa na vyumba vya kisasa na zoezi linaendelea wodi 19 na 20.

Pia,Jengo la Afya ya Akilli, Jengo la Utengamao pamoja na korido zote zimeboreshwa kwa kupigwa rangi lengo likiwa ni kuinua mandhari ya Hospitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles