33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yampongeza Kanali Ikangaa kuja na First Ladies

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Serikali imempongeza mwanariadha mkongwe nchini kuleta wazo la mashindano ya riadha ya wanawake maarufu First Ladies ambayo yanafanyika kila mwaka yakisikisha mikoa yote Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo leo Novemba 25, 2023, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro, amesema Kanali Ikangaa anastahili sifa kipindi hiki akiwa hai.

Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akiongoza mazoezi ya viungo katika uzinduzi huo.

Dk. Ndumbaro amesema mwanariadha huyo ameonesha kujali kukuza vipaji vya vijana kuliko kujiangalia yeye pekee kupitia fursa aliyopata kutoka Serikali ya Japani.

“Kanali Juma Ikangaa alivyoulizwa na Wajapani tukufanyie nini? Ingekuwa mwingine angesema ninunulieni gari au kusomeshewa watoto wake lakini ameona kitu muhimu ni kurithisha kipaji chake kwa vijana Kwa kuanziasha mashindano ya First Ladies.

“Sisi waswahili tuna tabia ta kumsifia mtu akishakufa, Mimi leo navunja huu mwiko. Leo naomba nimsifie Kwa dhati kabisa Kanali Juma Ikangaa kwa hiki alichofanya,”amesema Dk.Ndumbaro.

Aidha amesema Ili kumpa heshima zaidi, kuanzia leo mashindano hayo ambayo ni msimu wa tano tangu yameanzishwa, yaitwe Kwa jina la Juma Ikangaa First Ladies.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, amesema Kwa asilimia 80 gharama yake inachangiwa na Japan kupitia JICA na Baraza linatoa kiasi kilichobaki.

Naye mwakilishi wa JICA Tanzania, Ara Hitoshi amesema mashindano hayo yanatoa fursa hasa kwa wanawake uelewa wa kijinsi na kujitambua na kupata moyo wa kushiriki michezo mingine.

Katimu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Gerson Msigwa amesema kuanzia mwakani mashindano hayo yatakuwa na michezo mingi zaidi ikiwamo soka la wanawake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles