30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yalenga kuimarisha usawa  mapambano virusi vya UKIMWI

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene amepongeza Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Wizara ya Afya na Wizara ya TAMISEMI katika Mkakati wa kupambana na Ukimwi kama janga la kitaifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS Bi, Winnie Byanyima.

Waziri Simbachawene ameeleza hayo Novemba 29, 2022 jijini Dar es saalam, wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani yenye Kauli Mbiu ya Dangerous Inequalities iliyotolewa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ukimwi Duniani UNAIDS, Winnie Byanyima.

“Serikali imedhamiria kuweka usawa wa kijografia usawa kimazingira usawa kati ya watoto na wakubwa na usawa wa kiuchumi ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma sawa ili wasiathirike na wale walio athirika wapate huduma za matibabu lakini pia huduma sawasawa kuhakikisha wanaendesha maisha yao,” amesema Simbachawene.

Awali, akitoa taarifa hiyo Byanyima amesema Tanzania imejitahidi kupunguza ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kila Mwaka kwa miaka kumi mfululizo.

“Tanzania Imejitahidi kupunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI na imekuwa ikifanya vizuri katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI,” amesema Byanyima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles