24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yakunjua makucha hoteli za kitalii

Mwandishi Wetu- Serengeti

SERIKALI imeanza ukaguzi wa hoteli za kitalii ilizozibinafsisha  kwa wawekezaji na wale watakaobainika kuziendesha chini ya kiwango, watanyang’anywa na kupewa wawekezaji wengine.

Hatua hiyo, inafanyika kutokana na  kuwapo malalamiko kutoka kwa watalii na wadau mbalimbali wa utalii juu ya  huduma  zisizoridhisha zinazotolewa na hoteli hizo.

Akizungumza baada ya kukagua baadhi ya hoteli hizo,zikiwamo  Soronera na Lobo, zilizo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara, Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  alisema lengo la kubinafsishwa hoteli hizo ilikuwa  ni kuboresha huduma.

Alisema hata Hoteli ya Musoma na Ngorongoro Wildllife iliyopo ndani ya Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro, ni  miongoni mwa hoteli   zilizofanyiwa ukaguzi.

Alisema mwekezaji asiyefanya hivyo, atanyang’anywa umiliki ili apewe mwekezaji.

Alisema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya hoteli zilizobinafsishwa kukwepa kodi ya tozo ya huduma pamoja na kuwalipa wafanyakazi wazawa mishahara midogo, huku wale wa kigeni wakilipwa mishahara mikubwa kwa kazi ya aina moja.

Akizungumza baada ya kukagua hoteli hizo,Waziri Kanyasu alisema baadhi vitu alivyoviona ni pamoja na uchakavu wa miundombinu na udanganyifu wa idadi ya watalii wanaofikia kwenye hoteli hizo .

Alisema wizara  itapeleka idadi ya hoteli zitakazobainika kwenda kinyume  ili Msajiri wa Hazina  aweze kuzifutia  umiliki.

Kuhusu tozo ya huduma ya mapato, amezielekeza halmashauri mbalimbali, ikiwemo ya Serengeti kupata taarifa sahihi kutoka  Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ( TANAPA)

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Serengeti,Victor Tonesha  alisema changamoto inayoikabili halmashauri hiyo, ni ya  kushindwa kubaini kiwango halisi cha fedha zinazotolewa na Wawekezaji hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles