Serikali yakataa vyombo vya kimataifa kumsaka Mo Dewji

0
1557

AZIZA MASOUD NA GRACE SHITUNDU -DAR ES SALAAM


WAKATI leo zikiwa zinatimia saa 72 tangu bilionea Mohammed Dewji (Mo) atekwe nyara huku kiza kinene kikiwa bado kimetanda juu ya mahali alipo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi haliwezi kuomba msaada vyombo vya kimataifa vya uchunguzi kwakuwa bado hawajashindwa.

Kangi alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana baada ya kuulizwa na gazeti hili mara tu alipomaliza mkutano wake na waandishi wa habari aliouitisha kutoa tathmini ya matukio ya utekaji na upoteaji wa watu nchini.

Gazeti hili lilitaka kufahamu iwapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ipo tayari kuruhusu vyombo vya kimataifa kusaidia uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo kwakuwa tayari siku tatu zimekwishapita pasipo mafanikio yoyote.

Akijibu swali hilo Kangi alisema; “Hatuwezi kuruhusu vyombo vya kimataifa kufanya kazi ya uchunguzi wa tukio hilo kwa sa…

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here