26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yajizatiti kukabili virusi vya corona

Aveline Kitomary – Dar es Salaam

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa nchi iko katika hatari ya kupata mlipuko wa virusi vya corona kutokana na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati ya nchi ya China na Tanzania.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Ummy alisema hadi sasa hakuna mgonjwa aliyepatikana na virusi hivyo na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.

“Tuna kazi kubwa kama nchi ya kudhibiti mlipuko wa ‘corona virus’, bahati nzuri mpaka sasa hatujapata mgonjwa wa virusi hivyo, lakini tuko katika hatari ya kupata mlipuko mkubwa sana kutokana na mwingiliano.

“Kwahiyo tunapambana kuhakikisha virusi haviingii, tumeweka wataalamu maeneo yote ya mipaka na tunajiandaa kikamilifu kuzuia virusi hivyo, ila changamoto ni kuwa mtu anaweza akaingia nchini halafu hana dalili zozote, lakini akawa anaambukiza,” alisema Ummy.

Alisema watumishi wa wizara hiyo katika ngazi zote wanahangaika usiku na mchana ili kuhakikisha usalama katika mipaka na kutengeneza mazingira ya kukabiliana kuzuia virusi hivyo visiingie.

Mlipuko wa homa ya mafua makali umeikuba nchi za China, Thailand, Korea Kusini, Japan na Marekani kuanzia mwanzoni mwa Desemba mwaka jana.

Mapema jana Wizara ya Afya ya China, ilitangaza kuwa watu wengine 56 wamefariki dunia hivyo kufanya idadi ya waliofariki dunia hadi hivi sasa kufikia 360.

Ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingia na majimaji yenye virusi kutoka kwa mtu mmoja kwa kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa na mafua makali, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, kuathiri mapafu, kupumua kwa shida na hadi kifo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles