27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaja na njia ya kubana wanakwepa kuchukua hati za adhi kikopwa kodi

Na MWANDISHI WETU-SHINYANGA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema zaidi ya watu 900,000 michoro ya ramani ya viwanja vyao imeidhinishwa lakini hawajaichukua na kwamba kuanzia sasa siku 90 baada ya mchoro kuidhinishwa we- nye ardhi wataanza kupelekewa stak- abadhi za kulipa pango la ardhi.

Alisema watu ambao michoro yao imekamilika, endapo wange- fika katika ofisi husika kulipia na kuchukua hati za viwanja vyao na kulipa kodi ya ardhi, Serikali ingepata Sh bilioni 125.

Lukuvi alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Ar- dhi Mkoa wa Shinyanga ambapo sasa

wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wakifuatilia hati zao Simiyu na Tabora, watapata huduma za ardhi katika ofisi mpya za ardhi zi- lizozinduliwa mkoani Shinyanga.

Lukuvi alisema mwananchi am- baye atashindwa kufuatilia hati yake katika kipindi cha siku 90 atapele- kewa stakabadhi ya malipo kuanzia tangu kiwanja chake kilipopimwa na michoro yake kuidhinishwa.

‘’Wale wamiliki ambao watashindwa kufuatilia hati katika kipindi cha siku 90 wataanza ku- daiwa kodi ya pango la ardhi kuanzia pale ambapo kodi iliidhinishwa hata kama michoro hiyo ni ya tangu mwa- ka 1962 ataanza kuanzia hapo maana itakuwa ni uzembe,’’ aliongeza Luku- vi.. Alisema Mkoa wa Shinyanga una zaidi ya wananchi 65,000 ambao

michoro ya ramani na hati za viwanja vyao vimeidhinishwa lakini hawa- jafutilia katika ofisi za ardhi za wilaya ili wapatiwe hati na kuanza kulipa kodi ya ardhi na kuwataka kufanya hivyo ndani Siku 90.

Alisema Serikali inataka kila Mtanzania apate hati milki ya ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kuwa Serikali haikusanyi kodi ya ardhi kwa mtu ambaye hana hati na kuwataka wachukue hati zao ili Serikali ipate mapato na kutoa huduma katika sek- ta za barabara na hospitali.

Katika hatua nyingine Lukuvi alitoa hati ya kiwanja kwa Zainab Ketuba 77 ambaye amekuwa akikosa haki hiyo tangu mwaka 1978.

Akizungumza Mbele ya Lukuvi, Ketuba alisema alinyang’anywa ki- wanja chake tangu enzi za vita vya

Idd Amini na hali hiyo ilijitokeza ali- posafiri kwenda kushiriki msiba wa baba yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tel- ack, alisema kuanzishwa kwa ofisi ya ardhi Mkoa wa Shinyanga tayari ameanza kuona kupungua kwa migogoro ya ardhi Mkoani kwake.

“Kama Mkoa tutahakikisha tu- naleta utulivu na kutokana na kuan- zishwa kwa ofisi za ardhi katika Mkoa wa Shinyanga kwa kuwa migogoro itakuwa imepungua” alisema Telack.

Tayari zoezi la uzinduzi wa ofisi za ardhi mikoa mbalimbali limefanyi- ka katika mikoa kumi hapa Nchini na zoezi kama ili linaendelea katika mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Mara, Geita na Mkoa wa Kagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles