26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaita kazini waajiriwa wapya 477

Amina Omari – Tanga

SERIKALI imewaita kazini waajiriwa wapya 477 ambao watahudumu katika kada ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi), Selemani Jafo, alisema kuwa watumishi hao wataweza kusaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi katika sekta hiyo, hususani maeneo yenye uhitaji.

“Kama mnavyotambua Tamisemi iliomba kibali cha kutangaza nafasi za ajira za utumishi wa umma, na leo  (jana) tunashukuru kwa Serikali kutukubalia maombi yetu,” alisema Jafo.

Alisema kuwa wizara hiyo iliomba kibali cha ajira katika maeneo 14, ikiwemo idara ya utabibu, wauguzi, wataalamu wa mionzi pamoja na watoa tiba kwa vitendo.

“Jumla ya waombaji 20,237 waliomba maombi hayo huku 2,644 pekee ndio walionekana na sifa, huku 17,593 wakikosa sifa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo za kutokidhi vigezo vya kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo licha ya kuwa na uhitaji mkubwa katika idara ya mionzi ambayo ilikuwa inahitaji watumishi 44, walioomba walikuwa 46 na wenye sifa wakiwa ni 25 pekee.

Hivyo amewataka waombaji wote kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 kuanzia jana wakiwa na vyeti vyao halisi vya elimu ya sekondari na taaluma.

“Napenda nitamke wazi kuwa waombaji wote waliopata nafasi hakutakuwa na fursa ya kubadilisha kituo cha kazi kwani wakati wanaomba walisema wapo tayari kufanya kazi mahali popote,” alisema Jafo.

Hata hivyo alisema kuwa waombaji waliopata nafasi ambao watashindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi baada ya siku 14 hawatapewa nafasi hizo tena, watapewa wengine wenye uhitaji.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwapangia watumishi hao maeneo yenye uhitaji zaidi ili kuharakisha utoaji huduma kwa wananchi.

Alisema kuwa Serikali imejenga vituo vingi vya afya ambavyo vinahitaji watumishi kuanza kutoa huduma, hivyo ni vema kuzingatia maeneo yenye uhitaji wakati wa upangaji watumishi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles