25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaipongeza Internews kwa mradi wake wa Boresha Habari

*Yasema umesaidia kuleta mageuzi makubwa kwenye tasnia ya habari

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imesema Mradi wa Boresha Habari unaoratibiwa na Shirika la Internews Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani(USAID) na wadau wengine umekuwa na mafanikio makubwa kwani umesaidia kuimarisha vyombo vya habari nchini kwa kuwajengea uwezo wanahabari.

Pongeze hizo zimetolewa Julai 6, 2023 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano, Kundo Mathew, katika hafla ya kufunga mradi huo uliodumu kwa miaka sita kuanzia 2017 hadi 2023.

“Tangu kuanzishwa kwa mradi huu wa Boresha Habari mwaka 2017 chini ya Internews kumekuwa na mapinduzi makubwa kwa sababu wamekuwa wakifanya kazi ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya namna gani wanawaeza kutekeleza majukumu yao kwa kwa ufasaha na kwa kuzingatia misingi ya taaluma hii muhimu.

“Katika mradi huu wa boresha habari pia umeweza kutoa wigo wa mafunzo ya Fact Checking nyenzo ambayo imeweza kusaidia waandishi wengi kutekeleza makujumu yao kwa umakini mkubwa, hivyo tunaishukuru sana Internews na washirika wake kwa namna ambavyo wameweza kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha ustawi wa tasnia ya habari unaimarika,” amesema Methew.

Adiha, katika hatua nyingine, Methew ameahidi kuwa Serikali itaendela kufanyia kazi changamoto zinazoikabili sekta ya habari nchini ili kuwawezesha wanahabari kutekeleza majukumu yao kwa uhuru huku akisifu juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Itakumbukwa Juni 13, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari, ambapo kati ya mambo 22 yaliyoletwa na wadau, mambo tisa yalikubaliwa.

“Sisi Serikali tunajivunia hatua hii ya mabadiliko ya sheria, wapo wanaosema hakuna kilichofanyika. Hatuwezi kubadilisha kila kila kitu. Sheria zinapotungwa hazikamiliki ndio maana zinapitiwa kulingana na mahitaji yaliyopo,” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na maboresho hayo, Serikali sasa itaanza kutoa matangazo kwa vyombo vya habari kwa kuzingatia ushindani.

Mapema, akimkaribisha Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema miongoni mwa maboresho yaliyofanywa ni pamoja vifungu vinavyomwondolea mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo uwezo wa kuchagua vyombo vya habari vya kuwapa matangazo. “Sisi tunaovaa viatu ndio tunajua wapi panabana,” amesema Balile.

Awali, Msimamizi wa Mradi huo wa Boresha Habari, Agnes Kayuni alisema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa zaidi ya waandishi wa habari 5,000 nchi nzima huku akikiri kuwa yamekuwa na matokeo chanya.

Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa ambayo imekuwa miongoni mwa taasisi zilizonufaika na mradi huo, Nuzulack Dausen amesema mradi huo unakamilika katika wakati ambao waandishi wa habari nchini Tanzania wanahitaji mafunzo kuliko wakati mwingine wowote ule hususan ya Fact Checking.

“Pamoja na hayo, tumefanikiwa kutoa mafunzo ya uandishi wa takwimu(data) kwa zaidi ya waandishi wa habari 1,500 nchini kote jambo ambalo tunajivunia na kutupa moyo kama Nukta Africa,” amesema Dausen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles