Arodia Peter, Dodoma
Serikali imeingia mikataba ya awali na makampuni sita ya kununua korosho.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara na Viwanda, Joseph Kakunda bungeni leo, Mei 16, ambapo amesema serikali imeendelea kusaini mikataba ya awali na makampuni ya ununuzi wa korosho.
“Korosho zetu bado zina ubora, zimefanyiwa ukaguzi kwenye maghala wametuhakikishia kwamba hazijaharibika na bado zina ubora ule ule,” amesema Waziri Kakunda.
Hata hivyo Waziri huyo hakutaja majina ya kampuni hizo.