32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaiagiza WHI kugeukia Wilaya, Halmashauri mpya

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imeitaka Taasisi ya Nyumba ya Watumishi Housing Investment(WHI) kujikita kwenye maeneo ya Wilaya na Halmahauri mpya kwa ajili ya kusaidia makazi kwa watumishi wa Umma.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Septemba 27, 2022 jijini Dar es Salaam na Waziri Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama alipotembelea mradi wa WHI ulipo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam.

“Miji yetu inakua na kadri inavyokua watumishi wa umma wanapelekwa kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za halmashauri na wilaya mpya na maeneo mengine ikiwamo zahanati na hospitali, lakini uhaba wa nyumba kwa watumishi hawa bado ni mkubwa.

“Kwa hiyo nitoe agizo, pamoja na miradi mizuri ambayo mnaifanya kwenye majiji mbalimbali niwatake sasa mfike kwenye maeneo ya pembezoni ambako imekuwa ni changamoto kwa watumishi wetu kupata makazi mazuri.

“Kule tunaweka kufanya mambo mawili la kwanza kwenye Faida Fund tunaweza kuwahamasisha mamlaka ya serikaki za mitaa kwenye hizo mhalmahauri mpya na wilaya kujiunga na mfuko huu ninauhakika tunaweza kupata nafasi ya kuanza kujenga nyumba kwenye maeneo hayo mapya ya utawala,” amesema Mhagama.

Aidha, katika hatua nyingine Mhagama ameiagiza WHI kurejea mpango wa kushirikiana na mamlaka nyingine kwa ajili ya kupeleka huduma bora kwa nwatumishi waliko vijijini huku akihimiza kuongeza gawio serikalini.

“Hatua hiyo itakuwa ni motisha kubwa kwa watumishi wetu walioko vijijini. Jambo jingine mnapotoa gawio kwa wawekezaji msisahau kutoa gawio serikalini kwani kadri mnavyofanya hivyo ndio mnapata pia mikopo ya ya kuweza kuendeleza miradi ya ujenzi,” amesema Mhagama.

Mradi wa WHI, Magomeni Usalama.

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama ametoa wito kwa maofisa utumishi wanaoshughulika na utawala utumishi wa umma kuwaunganisha watumishi na WHI ili waweze kujua kuwa fursa ya makazi bora inapatikana.

“Kwani kama tunavyofahamu kwamba mtumishi yeyote wa umma anaweza kununua nyumba mahali popote pale hata kama ataitumia kwa ajili ya kujiongezea kipato bado lina manufaa,” amesema Mhagama.

Pia, imeitaka kujenga nyumba zitakazotumiwa na watumishi wa umma wanaostaafu baada ya kuwa wamelitumikia taifa.

Akizungumzia mradi huo wa Magomeni, Waziri Mhagama ametoa kipindi cha miezi sita kwa WHI kubadilisha matumizi ya sakafu ya kwanza(Floor ya kwanza) kutoka kuwa eneo la biashara hadi makazi.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WHI, Paskali Massawe akizungumzia mradi huo wa magomeni amesema nyumba zote 88 zimenunuliwa na watumishi wa umma huku akiahidi kufanya ukarabati nyumba nane za floor ya kwanza zitakazo fanya jumla ya nyumba katika jengo hilo kuwa 96.

“Changamoto yetu imekuwa ni mtaji ambapo tumekuwa tukiendelea kuzungumza na wawekezaji kwa ajili ya kuongeza mtaji.

“Kwasasa tuna kitengo chetu cha ujenzi ambacho kimefika daraja la kwanza hatua itakayopunguza gharama za ujenzi na uuzaji wa nyumba zetu kwa ujumla.

“Pia, tuna malengo ya kuendelea kujenga nyumba kwenye halmashauri mpya ambapo halmashauri za Mbeya na Songea zimeonyesha nia ya kutaka kufanya kazi na sisi,” amesema Massawe.

Utafiti unaonyesha kuwa nyumba zinazojengwa na kuuzwa na WHI zimekuwa na unafuu wa bei zaidi ya asilimia 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles