23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yagawa magari 130 yaliyotaifishwa

 MWANDISHI WETU – DODOMA 

RAIS Dk. John Magufuli ameagiza magari 130 yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi, yagawanywe kwa taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali. 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dodoma jana, baada ya kukagua magari hayo yaliyohifadhiwa kituo cha mabasi cha zamani jijini hapa. 

Magari hayo, yakiwamo makubwa na madogo, yalikamatwa maeneo mbalimbali nchini, kisha wahusika kufikishwa mahakamani. 

Taarifa hiyo ilisema mahakama ilitoa uamuzi wa kuyataifisha. 

Akizungumza baada ya kukagua, Rais Magufuli aliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata watu waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo, ikiwamo biashara haramu ya meno ya tembo. 

Pia taarifa hiyo ilisema Rais Magufuli aliwapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na aliwaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles