27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yafuta leseni 33,000 za madini, kuzigawa kwa wachimbaji wadogo

Bethsheba Wambura

Serikali imefuta leseni 33,000 za wafanyabiashara wa madini ambazo zinatarajiwa kugawiwa kwa wachimbaji wadogo.

Biteko amesema hayo leo Ijumaa Julai 5, wakati akizungumza mbele ya Rais Dk. John Magufuli na wananchi na wageni waalikwa katika mapokezi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata katika Uwanja wa Ndege wa Chato, mkoani Geita.

Amesema kuna madini nchini yanawanufaisha watu wa nje kitu ambacho Rais Magufuli likataa.

“Haiwezekani watu waje hapa kutoka nje kuchimba halafu watuache sisi na umaskini wetu hizo zilipendwa kwa wakati huu, kwa wazawa wenye nia njema ya uwekezaji katika madini kwa nia njema wanakaribishwa.

“Naomba nitoe wito kwa Watanzania wote ambao walikuwa wanatorosha madini kwenda nje waache mara moja kwani wanatukera na hakuna heshima yoyote unayoipata kuibia nchi yako na kupeleka nchi nyingine,” amesema.

Pamoja na mambo mengine Biteko amesema  wizara yake imelenga kukusanya hadi Sh bilioni 470 katika madini yote nchini mwaka huu.

 “Tulikuwa tunapata Sh bilioni 190 kutoka kwenye madini lakini hivi sasa tunapata bilioni 350 na kwa maelekezo ya Rais tutapokea hadi bilioni 470 hadi kufikia mwaka 2020,” amesema Biteko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles