25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yafunguliwa kesi 13 nje kwa miaka mitatu, yadaiwa Dola milioni 189.58

Mwandishi Wetu, Dodoma



Jumla ya mashauri 13 yamefunguliwa nje ya nchi dhidi ya Serikali tangu Novemba mwaka 2015 huku madai kwenye mashauri hayo yakiwa Dola za Marekani 185,580,009.76.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Novemba 9 na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Katika swali lake la msingi, Zitto alisema Tanzania inakabiliwa na mashauri mashauri mbalimbali kwenye za kimataifa kama vile ICSID, ICA London pamoja na ICC Paris huku akitaka kujua idadi ya mshauri yaliyofunguliwa nje dhidi ya serikali.

“Kuanzia Novemba 2015, mashauri hayo ni mangapi kwa idadi, kwenye mahakama zipi na je jumla ya madai ya mashauri hayo yote ni kiasi gani cha fedha kwa dola za Marekani na kuanzia mwaka 2000-2018 kumekuwa na mashauri mangapi dhidi ya Jamhuri, mangapi yameamualiwa, mangapi bado na mangapi Tanzania ilishinda.

“Je kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Acacia Minging (LCIA Arbitration No. UN 173686 No. 87) huko London Uingereza ina madai gani, na je kwanini kuwe na kesi mahakamani wakati Serikali ilifanya mazungumzo na Barrick Gold ambao ni wamiliki wa Acacia?” amehoji Zitto.

Akijibu maswali hayo, Profesa Kabudi alisema mashauri yaliyofunguliwa kuanzia Novemba 2015  ni 13 na yapo kwenye mahakama za usuluhishi za Permanent Court of Arbitration (PCA), London Court of International Arbitration (LCIA), International Center for Settlement of Investment Dispute (ICSID) na huko Johannesburg Afrika Kusini kupitia Sekretariet ya UNICTRAL.

“Jumla ya madai katika katika mashauri hayo ni Dola za Marekani 185,580,009,76. Mashauri yote kwenye mahakama za kimataifa bado hayajatolewa uamuzi, hivyo takwimu halisi za madai na gharama ambazo Serikali inaweza kuwajibika kulipa itapatikana baada ya mashauri kuhusu kukamilika na uamuzi kutolewa.

“Kwa sasa hakuna kesi yoyote katika mahakama ya usuluhishi London iliyofunguliwa dhidi ya Serikali na kampuni ya Acacia Mining Llc. Shauri Na. LCIA Arbitration UN 173686 lililotajwa na shauri UN 1736867 yamefunguliwa Julai 3, 201  na kampuni za Pangea Minerals Limited na Bulyanhulu Gold Mining Limited.

“Utetezi wa Serikali kwenye kesi hizo umeshawasilishwa mahakamani. Makampuni hayo yameendelea na mashauri hayo kwa madai ya kulinda maslahi ya wanahisa hao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles