24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaeleza mkandarasi Kinyerezi I alivyofilisika

FARAJA MASINDE – DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema imeamua kuvunja mkataba na mkandarasi aliyekuwa akitekeleza mradi wakufua umeme wa Kinyerezi I baada ya kufilisika. 

Hayo yalisemwa jana  na Waziri wa Nishati, Dk. Merdadi Kalemani, wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini baada ya kutembelea mradi huo uliopo Tabata Kinyerezi  jijini Dar es Salaam.

Alisema hadi kufikia kuvunja mkaba huo mkandarasi huyo alikuwa ametekeleza asilimia 84 ya kazi huku akiwa tayari amelipwa asilimia 60 ya malipo. 

“Tuliamua kuvunja mkataba na mkandarasi ambaye ni Jacobson kutoka Norway baada ya kudai kuwa amefilisika,  hivyo serikali ilichukua suala hili kwa kushirikiana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, vyombo vya dola na Tanesco, tulihakikisha kuwa jambo hilo halileti athari kwetu. 

“Hivyo Machi 2, mwaka huu tukaamua kuvunja mkataba rasmi baada ya kupokea maelekezo kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu, pia serikali inaendelea kufuatilia nchini Norway iwapo kutatokea suala lolote lenye kutuathiri kufuatia kufilisika kwa mkandarasi husika.

“Mradi huu ambao utagharimu dola milioni 188, ni muhimu sana kwetu na ndiyo maana Septemba mwaka jana nilitembelea mradi huu na kuwashikilia wakandarasi waliokuwa wamebaki katika kujiridhisha iwapo vifaa viko salama kwa kushirikiana na vyombo vya dola jambo ambalo lilikuwa sahihi,” alisema Dk. Kalemani. 

Alisema kuwa tayari ametoa maelekezo kwa Shirika  la Umeme Tanzania (Tanesco) na mamlaka zinazohusika kuhakikisha ndani ya siku 30 wanakuwa wamepata mkandarasi atakayekamilisha mradi huo na kwamba matazamio ya wizara ni kuona kazi hiyo inakamilika si zaidi ya miezi sita.

“Miradi hii miwili ya Kinyerezi I na II kwa sasa zinazalisha megawati 388 ambapo Kinyerezi l tunafanya upanuzi lengo likiwa ni kuongeza megawati 185, hivyo mradi huu ni muhimu sana kwetu,” alisema Dk. Kalemani. 

Waziri Kalemani alisema kuwa kazi kubwa ya mkandarasi huyo ilikuwa ni upanuzi wa kituo kwa kufunga mitambo mikubwa minne ili kuongeza megawati hizo,  pia kuunganisha miradi yote miwili ya Kinyerezi l na ll kwa kujenga njia ya kusafirisha umeme wa KV 220 ambayo imekamilika.

Pia kazi nyingine ilikuwa ni kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi l kwenda Kituo cha kufua umeme cha Gongo la Mboto ambayo tayari imekamilika. 

Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula, alisema kuwa wameridhishw ana namna serikali ilivyoshughulikia suala la kuvunja mkabata na mkandarasi wa awali huku ikipongeza namna mradi huo unavyotekelezwa.

“Ni kweli kwamba tumetembelea mradi huu wa Kinyerezi I awamu ya pili ambao ulikuwa unaenda kutupa megawati 180 za ziada ukiacha zile megawati 150 ambazo zilikuwa zimekamilika na tulitegemea uwe umekamilika mwaka janalakini hapa katikati tulipata matatizo kwa mkandarasi ambaye alipewa kazi hii kufilisika,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles