26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaeleza chanzo watu 53 kulazwa

Na  AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsi Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile asemakuwa mpaka sasa jumla ya watu 53 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kula chakula msibani na kupata madhara kiafya .

Akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ndugulile alisema  dalili zilizoonekana kwa watu haoni ni kuumwa tumbo ,kuharisha ,homa na kutapika .

“Tukio la mlipuko wa magonjwa ya kuhara Kata ya Mtumba mji wa Serikali, ulianza Disemba 14, mwaka huu  baada ya wathirika kushiriki msiba katika mtaa huo,mara baada ya kula chakula  dalili zilizoonekana ni kuumwa tumbo,kuharisha,homa kutapika ,kuumwa. 

“Wagonjwa 53,wamelazwa hospitalini, huku wanaume 12, wanawake 41 na watoto 5 mpaka sasa hakuna kifo kilichotokea na wagonjwa wote wanaendelea na matibabu na hali zao ni nzuri wengine  wataruhusiwa kutoka hospitali siku ya leo (jana) ,”alisema.

Alisema Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  imepeleka timu ya wataalamu ili kuchunguza na kubaini chanzo cha mlipuko huo.  

“Wizara kwa kushirikiana  na timu ya usimamizi wa  afya Mkoa wa  Dodoma, ilipeleka timu ya wataalamu  kubaini chanzo cha mlipuko huo timu hiyo  imejumuisha wataalamu kutoka  wizara yangu, mkemia mkuu, mkoa wa Dodoma,TBS  na sampuli za chakula, damu na choo zilichukuliwa sehemu ambapo mlipuko ulipotokea,”alieleza.

Aliwataka wananchi kuzingatia kanuni za afya hasa katika mikusanyiko ya watu ,aliitaka mikoa na halimashauri kutoa taarifa kwa haraka na kwautaratibu uliowekwa pindi magonjwa yanapotokea.

“Wananchi wanatakiwa kuhakikisha katika mikusanyiko kama vile sherehe na misiba  uwapo wa maji safi na salama ,huduma za vyoo na kula vyakula vya moto hii ni changamoto kwani vyakula vinapikwa muda mrefu na kupoa maeneo hayo.

“Natoa wito kwa mikoa na halmashauri yote nchini kutoa taarifa kwa za mgonjwa kwa kutumia mfumo wa utoaji taarifa za magonjwa ya mlipuko pamoja na taarifa za afya kwa umma pia wananchi wazingatie kanuni za afya bora kujenga vyoo bora ,kuchemsha maji au kutibu ,kuandaa chakula katika mazingira bora.

Akizungumzia  kuhusu taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii, inayoeleza kuwepo mlipuko wa ugonjwa mpya unaofafana na malaria, Ndugulile alisema hakuna mlipuko wowote wa magonjwa uliotokea kwasasa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles