24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaanzisha utalii wa fukwe ziwa Viktoria

Anna Potinus – Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala amesema wameanzisha utalii wa fukwe katika ziwa Viktoria na kwamba tayari Mamlaka ya hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) inajenga kivuko kitakachokuwa na uwezo wa kupakia magari manne hadi sita na abiria wasiopungua 100.

Kigwangala ameyasema hayo leo Jumanne Julai 9, wilayani Chato mkoani Geita katika hafla ya uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702 ambapo amesema kuwa kuna wanyama waliokuwepo katika hifadhi hiyo na baadae wakatoweka hivyo watafanya jitihada za kuwarudisha katika makazi yao ya asili.

“Katika mapori haya kulikuwa ma Faru lakini walitoweka na tunajua aina ya Faru waliokuwepo hapa hivyo tutafanya jitihada za kuwarudisha katika makazi yao, pia tunatarajia kupokea faru 10 wenye asili ya Tanzania kutoka nchi za nje kuja kuongeza idadi ya faru katika nchi yetu,” amesema.

Aidha amesema kuwa wapopandisha hadhi mapori hayo uwindaji utakoma na matumizi yatabadilika na kwamba kiwango cha ulinzi na uhifadhi kitaongezeka kwa kiwango cha juu.

“Katika kipindi ambacho uvamizi ulikuwa umetamalaki wanyama wengi walitoweka lakini tangu tumepandisha hadhi mapori haya idadi imeanza kurudi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles