33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAANZA UCHUNGUZI SAKATA LA MWANAMKE ALIYEJIFUNGULIA KITUO CHA POLISI

Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imesema imefungua jalada la uchunguzi kuhusu mwanamke aliyejifungua sakafuni katika kituo cha polisi Mang’ula wilayani Kilombero katika Mkoa wa Morogoro,  Amina Mapunda.

Soma zaidi… http://mtanzania.co.tz/simulizi-ya-kuhuzunisha-aliyejifungua-akiwa-polisi/

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusuph Hamad Masauni alipotakiwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kutoa ufafanuzi wa Serikali kuhusiana na suala hilo.

“Tukio lililotokea huko Morogoro ni la ovyo kabisa na la kinyama na Serikali mnaweza kutoa kauli hapa na taifa likasikia,” amesema Chenge.

Akitoa kauli ya Serikali, Masauni amesema tayari jalada la uchunguzi limefunguliwa ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.

“Tukio hilo lilimhusisha mume wa huyu mama ambaye alinunua kitanda cha wizi na polisi walipokwenda kwake wakakuta hicho kitanda cha wizi.

“Hivyo wakamkuta mke wake wakamchukua kwa ajili ya mahojiano, kitu ambacho hakikuwa sawa katika mazingira ya kawaida busara ingetumika.

“Hivyo serikali tumelichukulia kwa uzito suala hili na tunaendelea na uchunguzi halafu hatua kali zitachukuliwa,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ni jambo lakusikitisha sana pale ambapo taasisi yenye mamlaka ya kulinda raia ndiyo inayoonekana ikisusika na upokonyaji na mauaji ya raia.
    Katika miaka ya hivi karibuni vitendo vya kikatili na mauaji vinavyofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia tanzania vimekuwa vingi sana. Kuna haja ya serilkali kuliangalia swala hili kwa undani. Watu kufia mikononi mwa polisi, mama kuzalia polisi nakadhalika ni matukio yasiyo na mwisho. Ipo haja ya kuangalia ni kwanini haya yahnatokea. Hata tukiwaadhibu polisi mmoja mmoja wanaofanya hivyo tatizo hili halitaisha. Tatizo hili linaenda ndani zaidi. Tatizo hili pengine nilakitaasisi (institutional). Ipo haja ya kuangalia upya Mafunzo ya polisi,Usimamamizi wa kazi zao, sheria na taratibu za kazi za polisi na elimu kwa raia kuhusu haki zao pale wanapokamatwa na polisi. Bila kufanya hivi taifa letu litaingia kwenye matatizo isiyotegemea

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles