23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaahidi kuwasaidia Wahandisi wazawa

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho, amesema Serikali itahakikisha sheria ya Local Content inazingatiwa na kuboreshwa ili kusaidia Wahandisi wazawa waweze kushiriki kikamilifu hasa katika miradi mikubwa na pale itakapohitajika ndipo itawatumia wataalamu kutoka nje ya Nchi.

Pia, amewataka Wahandisi hao kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ikiwa ni pamoja na  kukamilisha miradi vizuri na kwa wakati pamoja na thamani halisi ya fedha ili weze kuonekana.

Akizungumza Septemba 2, 2021 jijini Dodoma katika mkutano wa 18 wa maadhimisho ya siku ya Wahandisi kwa mwaka 2021, ambao ulienda sambamba na kula kiapo kwa Wahandisi wapya 630 kula kiapo cha uadilifu katika utumishi, Waziri Chamuriho amesema ili kuhakikisha ushiriki wa Watanzania wengi zaidi na kufikia malengo kwa haraka utekelezaji wa miradi haunabudi kushirikisha sekta binafsi ikihusisha wakandarasi wa kizalendo.

Amesema serikali itahakikisha sheria ya Local Content inazingatiwa na kuboreshwa ili kuhakikisha Wahandisi wazawa waweze kushiriki kikamilifu hasa katika miradi mikubwa na pale itakapohitajika ndipo itawatumia wataalamu kutoka nje ya Nchi.

“Jambo muhimu ninalopenda kusisitiza kwenu ni kuwepo kwa utayari wenu na kuhakikisha kwamba mnajijengea uwezo unaohitajika ili muweze kuzitumia fursa hizi kikamilifu,” amesema Waziri Chamuriho.

Vilevile, amewataka Wahandisi hao kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi vizuri na kwa wakati pamoja na thamani halisi ya fedha iweze kuonekana.

Aidha, amezitaka Taasisi binafsi na za umma pamoja na sekta binafsi kuwatumia vijana wanaomaliza vyuo ili waweze kupata uzoefu wa kazi.

Kuhusiana na kazi nyingi kupewa makampuni ya nje,Waziri Chamuriho amesema jambo hilo wamelipokea na watalifanyia kazi kuhakikisha miradi mingi wanapewa wazawa ili fedha ziweze kubaki nchini.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo anaeshughulikia ujenzi,Mhandisi Josephu Mwalongo amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana mawazo,kufanya tathmini ya mkutano wa 17,majadilino ya kitaaluma pamoja na michango mbalimbali ambayo wamefanya Wahandisi nchini.

Naye,Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Prof.Ninatubu Lema amesema wanakabiliwa na changamoto za matumizi ya force akaunti katika miradi mingi hivyo kuwanyima fursa ya kutekeleza miradi kwa ufanisi,pamoja na miradi mingi kutelezwa na Makampuni kutoka nje hivyo kuwanyima fursa vijana na makampuni ya Kitanzania.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda Vijijini,Selemani Kakoso amewataka wahandisi nchini wasiende kudhalilisha taaluma zao kwa kufanya miradi chini ya kiwango,pamoja na kuwa na umoja.

“Naiomba Serikali yangu kuwawezesha wahandisi ili waweze kukamilisha miradi kwani kwa kipindi cha miaka mitano Serikali imetoa zaidi ya shilingi  trilioni 20 na nyingi zimeenda nje ya nchi hivyo ni lazima tuwawezeshe wa hapa nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles