30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaahidi kukamlisha mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe

Safina Sarwatt, Mwanga

Serikali imeahidi kukamilisha mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe unaogharimu zaidi ya Sh billion 262 ndani ya miezi 14 ili kuondoa adha ya kero ya maji ya muda mrefu kwa wananchi katika wilaya za Mwanga,S ame na Korogwe.

Hayo yameelezwa na Waziri wa maji, Juma Aweso, Machi 13, 2023 Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla ya utiaji saini uhuishaji wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kati ya wizara ya maji na kampuni ya M.A Kharafi & Sons ambao watahusika kwa upande wa chanzo, kutibu maji na kulaza bomba kilometa 10.

Waziri Aweso amesema kumekuwepo na ucheleweshwaji wa utekelezaji wa mradi huo na kwamba tayari hatua zimeshachukuliwa kukamilisha ambapo alisema kazi kubwa tayari imekwishafanyika na ndani ya meizi 14 Wananchi watapata huduma ya maji safi na salama.

“Nakiri mradi huo kuchelewa katika utekekezaji hali ambayo imewakatisha tamaa wananchi na hata viongozzi lakini sasa serikali imeupa kipaumbele kuhakikisha unakamilika na wananchi wanaondokana na adha ya maji,”amesema Aweso.

Amesema wakandarasi na viongozi wa wizara hakuna mwenye kisingizio kuhusu utekekezaji wa mradi huo, na kwamba kazi iliyobaki ni kwenda kwenye usimamizi na utekekezaji wa mradi.

“Pia mkandarasi tumempa muda wa miezi 14 kukamilisha mradi huu, sasa atupe chati kutueleza kila mwezi atatekeleza kwa asilimia ngapi ili viongozi watakapofika kukagua waweze kuwabanana na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi kwa wakati,” amesema Aweso.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nadhifa Kemikimba amesema mradi huo umechukua muda mrefu na kwamba kwa sasa wizara imejipanga kuhakikisha unakamilika na wananchi wanapata maji.

Naye Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo amesema mradi huo ukikamilika utaondoa kero ya upatikanaji wa maji katika mji wa Mwanga na maeneo mengine ya Tambarare.

Amesema pamoja na mradi huo pia ipo miradi mingine ya maji inayotekelezwa katika Wilaya hiyo, lakini kasi yake bado si ya kuridhisha.

Mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh bilioni 262 hadi kukamilika kwake, ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ambapo ulipaswa kukamilika 2017, utanufaisha zaidi ya wananchi 438,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles