27.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Serikali yaahidi kuendeleza ajenda za maendeleo zilizoachwa na Ruge

Elizabeth Joachim- Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jeneral Marco Gaguti amesema anaungana na Watanzania katika kuendeleza ajenda za maendeleo ikiwa ni njia ya kumuenzi aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo leo Jumatatu Machi 4 wakati akitoa salamu za rambi rambi katika viwanja vya Gymkana Mjini Bukoba wakati wa ibada ya mwisho ya kumuaga mkurugenzi huyo.

“Nilikutana na Ruge, Agosti 2 mwaka jana na alivyoniona alifurahi sana alisema amefurahia vijana kupewa nafasi katika uongozi na tukapanga kufanya jambo kuhusu Mkoa wetu wa Kagera”

“Tangu siku ile sijaonana na Ruge tena mpaka leo, ila naahidi kuungana na watanzania wenzangu kufanya yale yote aliyoyaacha ikiwa ni njia ya kumuenzi,” amesema Gaguti.

Ruge Mutahaba amezikwa leo kijiji cha Kiziri Mjini Buboka na mazishi yake kuudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Januari Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Wasanii mbalimbali na wananchi kutoka mikoa mbalimbali

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles