30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Serikali yaagiza kulindwa mazingira milima Uluguru

 MWANDISHI WETU – MOROGORO 

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Sima amemuagiza uongozi wa Mkoa wa Morogoro, kuandaa kikao ndani ya siku wiki moja na kukutana na viongozi wa wilaya za mkoa huo pamoja na wadau wa mazingira kujadili juu ya utatuzi wa changamoto za mazingira katika milima ya Uluguru. 

Ahizo hilo alilitoa juzi baada ya kupokea taarifa fupi ya mkoa kuhusu utunzaji wa mazingira katika milima hiyo ilivyo akiwa katika ziara yake ya kukagua mazingira mkoani humo na kuwataka wafanye kikao hicho kitakacholeta mapendekezo sahihi ya namna ya kulinda mazingira yasiharibike kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea katika milima ya uluguru. 

“Safu ya milima ya Uluguru ni chanzo cha maji mkoani Morogoro hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira katika milima hiyo inahifadhiwa na kulindwa kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae,” alisema Waziri Sima 

Alisema kuwa magonjwa ya milipuko yanatokana na utiririshaji wa maji taka kwenye vyanzo vya maji yamekua ni mengi hatua stahiki na za haraka zichukuliwe ili kulinda watu pamoja na milima hii ya aina yake katika nchi yetu. 

“Wadau wote wa Mazingira pamoja na viongozi wa ngazi za Watendaji wa mtaa, kata na vijiji washiriki kwenye kikao cha pamoja kujadili na kuangalia namna bora ya kutatua changamoto ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika milima ya Uluguru na repoti hiyo ifike katika ofisi ya makamu wa rais kwa hatua zaidi,” alisema Waziri Sima

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles